Jacline akiongea kwa ridhaa ya mama yake amesema alipigwa kwa kutumia
ubao na mwalimu wa shule hiyo Novemba 19 mwaka huu na mwalimu Kanyika
kwa kosa la kuwa na nywele ndefu.
Mwanafunzi huyo amedai kuwa siku ya tukio alipigwa vibaya na
kumsababishia maumivu makali ambapo siku hiyo mama yake alikuwa safarini
Nairobi Kenya hivyo hakupata matibabu ambapo alilazimika kumwambia
mwalimu jirani[Bibi]ambaye alimpeleka hospitali kutibiwa.
Picha ya X ray ikionesha kidole kilichovunjika :
Hata hivyo Jackline amesema kuwa kutokana na maumivu makali alilazimika
kufanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne bila kupata matibabu ya
kutosha.
Baada ya kurejea kutoka safari mama yake mzazi aitwae Rehema Adamson
Ndeje[28] mkazi wa Block T jijini Mbeya amesema baada ya maumivu ya
mwanae usiku ilimlazimu kwenda shuleni ili kujua kulikoni,ndipo
alipoonana na mwalimu Kanyika baada ya kukutanishwa na Mwalimu mkuu.
Mama Jackine amesema hicho ni kipigo cha tatu kukubwa kwa mwanae kupigwa
na mwalimu huyo ambapo alionesha makovu yaliyodaiwa yalitokana na
vipigo vya mwalimu huyo miguuni akidai majeraha hayo yalidumu kwa miezi
mitatu.
Hata hivyo Rehema aliamua kwenda Polisi Mwanjelwa kutoa taarifa za tukio
na kila alipoitwa mwalimu huyo hakutokea ndipo jalada likapelekwa kituo
kikuu cha kati ambapo mwalimu alikamatwa na mhanga kupewa PF 3 kwa
ajili ya matibabu ambapo alipigwa picha na kuonekana moja ya kidole cha
kati cha kushoto kimeathirika kutokana na kupigwa kwa kutumia ubao.
Mzazi huyo amesema hana nia mbaya na mwalimu Kanyika lakini kitendo cha
kumwadhibu mwanae mara kwa mara ndicho kimemtia shaka hata kuamua kutoa
taarifa Polisi ili sheria ichukue mkondo wake.
Mwandishi wa habari hii alipofika shuleni ili kujua mustakabali wa suala
hili, mwalimu alimtoa nje akidai yeye ana majukumu mengine .
Mwandishi alimtafuta mmoja wa wanaharakati wa kijinsia ambaye alikiri
kupokea lalamiko hilo ingawa alijibu kwa mkato kuwa mtoto huyo kaumia
kidogo tu na ni usanii mtoto huyo kufungwa POP na kwamba bado PF3
haijajazwa kitu hivyo hawezi kuzungumzia lolote.
Kumekuwa na malamiko mengi katika Dawati hilo kutokana na matukio
kutochunguzwa kwa wakati , hali inayotoa mwanya kwa vitendo hivyo
kuibuka mara kwa mara na wahalifu kutoroka mkono wa sheria .
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya ameahidi kulifuatilia suala hilo na
ikibainika mtuhumiwea atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma
zinazomkabili.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu