Mtoto Benson Tole akiwa na mama yake |
MTOTO Mmoja
BENSON TOLE mwenye umri wa miaka Mitano mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea
mkoani Ruvuma, amenusurika kifo baada ya kukatwakatwa kwa kitu chenye
ncha kali sehemu za usoni na Mzee mmoja LONGINUS HAULE mwenye miaka 51
akimtuhumu mtoto huyo kumuibia matunda aina ya Mapera shambani kwake.
Mtoto BENSON
TOLE kwa sasa amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Songea katika
chumba cha uangalizi maalumu (ICU), Madaktari wanaendelea kunusuru uhai
wa mtoto huyu baada ya kupata mashambulio makali ya kucharangwacharangwa
na kitu chenye ncha kali sehemu za usoni na mtuhumiwa mmoja LONGINUS
HAULE mkazi wa Polisi Lizaboni mjini Songea.
Mzee HAULE
anatuhumiwa baada ya kumfanyia unyama wa kutosha mtoto huyo na kisha
kupoteza fahamu akimtuhumu kumuibia matunda aina ya mapera shambani
kwake alimtupia kwenye nyumba moja ambayo haijaisha ujenzi wake akidhani
tayari ameshamuua.
Afisa Muuguzi wa
Hospitali ya mkoa mjini Songea, JOSEPH MTEWELE amesema kwa sasa mtoto
huyo yupo chini ya uangalizi maalumu na kwamba madaktari wanaendelea na
jitihada za kunusuru uhai wake kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata
sehemu za kichwani. Jeshi la polisi mkoani Ruvuma limetihibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba linaendelea kuchukua hatua zaidi za
kumfikisha Mzee LONGINUS HAULE kwenye vyombo vya sheria kwa hatua
zaidi.
Credit: Emmanuel Msigwa Channel Ten Songea.