NAIBU
wa Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia January Makamba ametaka
ujio wake Jiji la Mwanza usihusishwe na Kampeni za chini kwa chini za
Urais bali ni kutekeleza ombi la Umoja wa waendesha pikipiki Mkoa wa
Mwanza kuwasaidia kupata Bima ya Afya baada ya kuwawezesha kupata
pikipiki 1745 za FEKON na si vinginevyo.
Kauli hiyo ya Makamba
ameitoa leo wakati wa kufungua kongamano kubwa la siku moja la Umoja wa
Madereva wa pikipiki Mwanza lililofanyika katika uwanja wa michezo wa
Nyamagana Jijini hapa, alisema kwamba kuna baadhi ya watu wameanza
kuhoji ujio wangu Mwanza “Niko hapa kwa ajili ya shughuli hii
mliyonialika bali kuja kushiriki Kampeni muhimu ya Bima ya Afya kwa
ajili ya Usalama wa badae” na si vinginevyo.
Makamba amesema kwamba
upatikanaji wa Leseni kwa urahisi na uharaka usiwe tiketi ya Kifo kwa
wananchi (ZAIDI MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY)
|
Awali
kabla ya kongamano hilo madereva hao wa bodaboda walifanya maandamano
toka makao makuu ya ofisi zao yaliyopo mtaa wa malango mmoja wilayani
Nyamagana jijini Mwanza hadi katika uwanja wa historia wa Nyamagana. |
|
Wadau wa Bodaboda wakiingia uwanja wa Nyamagana. |
|
Ndani ya uwanja wa Nyamagana madereva wa Bodaboda wamejitokeza kiasi cha kutosha. |
|
Huku wengine wakizidi kumiminika viwanjani hapa kuhudhuria kongamano lao. |
|
Naibu
wa Sayansi na Teknolijia ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli mhe. January
Makamba akiingia katika uwanja wa Nyamagana kushiriki kongamano la Bima
ya Afya kwa waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda wa mkoa wa Mwanza. |
|
Kila mmoja viwanjani hapa alikuwa na kiu ya kusalimiana ana kwa ana na Naibu waziri huyo. |
|
Licha
ya kutoa elimu ya uelimishaji kujitambua kwa Bodaboda wa jiji la Mwanza
ili kuepukana na maisha magumu uzeeni kwa wadau hao wa usafiri, Mkuu wa
mkoa waMwanza Evarist Ndikilo ndiye aliye mkaribisha Mhe. Naibu waziri
wa Sayansi na Teknolojia kuhutubia maelfu ya wadau hao. |
|
Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza Injinia Evaris Ndikilo kabla ya kumkalibisha mgeni
rasmi aliwaasa bodaboda kufuata sheria na kanuni ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha shughuli zao zinafanyika kwa umakini na kwa amani na utulivu huku
wakihakikisha usalama kwanza katika kazi zao kwa kuwa wanatumia vyombo vya
moto.
Injinia Ndikilo
aliwataka pia kufuata sheria za barabarani kutokana na kuwepo watumiaji
wengine, kuwa waangalifu na abiria wengine wanaowachukua kutokana na baadhi yao
kuwateka na kuwafanyia ukatili, kuwauwa na kuwanyanganya pikipiki zao nyakati
za usiku na kuwataka kukataa kushiriki katika shughuli za uhalifu na badala
yake wawabaini na kuwatolea taarifa kwa viongozi na jeshi la polisi.
|
|
Makamba
alisema kuwa kupatikana kwa Bima za Afya kutatawezesha wanaopata ajali
kupatiwa matibabu na kupata fidia pindi wanapopata ajali na kupata
ulemavu na kifo jambo ambalo ni hakika lazima wakubali kukata bima
kutoka Kampuni ya Ndege Insurance na Shirika la Bima la Taifa (NIC)
yaliyokubali kuingia mkataba na wa waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza. |
|
Ametoa wito kwa Jeshi la
Polisi kuachana na tabia ya manyanyaso kwa waendesha pikipiki ya kuwabambikia
kesi na makosa bali washirikiane nao kuwabaini walio wachache wanaojipenyeza
kujifanya ni bodaboda kumbe ni wanaofanya vitendo vya kihuni, uhalifu na wizi
kwa kivuli cha bodaboda jambo ambalo litasaidia pia kuwabaini wanaovunja sheria
taritibu zilizopo.
|
|
“Mimi leo nimekubali kuwa Mlezi wenu lakini kila kijana lazima amiliki
pikipiki yake mwenyewe badala ya kuwa mtu wa kuajiliwa tunahitaji kila mmoja
ajiajili kwa kuwa na chombo chake, kazi ya pikipiki iwe ya usalama isiwe leseni
ya kifo na ulemavu, msije mkadanganywa na baadhi ya watu kuwa watawatetea bali
sisi wa viongozi wa Serikali Taifa, Mkoa, Wilaya na Jiji na kuweni makini kwa
kufuata sheria za usalama” alisisitiza |
|
Tangu kuingia mkataba na Kampuni ya Tanzania China Dev Ltd wamefanikiwa
kuwakopesha 1745 na awamu ya kwanza umoja umlikopesha pikipiki 265, awamu ya
pili 450 na awamu ya tatu pikipiki 1000 na wanachama wapatao 1745 wamenufaika
na kupata ajira . |
|
Mstahiki
meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula alikuwa ni mmoja kati ya
viongozi walioshiriki zoezi la kuendesha bahati nasibu ya waendesha
bodaboda 100 waliobahatika kuandikishwa Bima ya Afya bure katika
kongamano hilo. |
|
Zoezi la bahati nasibu ya Bima ya Afya linaendelea na waliobahatika ndiyo hawa waliokuwa wakifika mbele katika mstari. |
|
Mwakilishi toka jeshi la polisi na bahati nasibu ya Bima ya Afya. |
Kongamano hilo limelenga
kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya kufuata sheria za usalama barabarani,
kusoma na kupata cheti na hatimaye leseni, kuhimiza kuvaa kofia ngumu, kuhimiza
kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuhimiza waendesha pikipiki kufuata
taratibu zote zilizowekwa na serikali kwa wanachama wa wilaya za Sengerema,
Nyamagana, Ilemela , Kwimba, Ukerewe, Magu na Misungwi.
|
Ndikilo kusanyikoni. |
|
Burudani ndani ya Kongamano hazikukosekana. |
|
Wadau walikuja na vyombo vyao. |
|
No Parking. |