Stori: Imelda Mtema na Richard Bukos
KICHEKO! Ile kesi ya kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni Meneja wa
Hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe Beach, Dar, Godlucky Kayombo
iliyokuwa ikimkabili Wema Isaac Sepetu imetolewa hukumu yake kama
ilivyokuwa ile ya shosti’ake, Kajala Masanja.
Wema Sepetu akitinga Mahakama ya Mwanzo ya Kawe, Dar.
Habari kutoka kwa chanzo makini cha gazeti hili kilieleza kuwa Wema alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu au faini ya shilingi laki moja kwa maana ya elfu hamsini kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia ya kutenda makosa hayo mawili ya kupiga na kutukana.
WEMA AOMBA IHARAKISHWE
Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu wa Wema au Madam zilieleza kuwa hukumu ya kesi hiyo ilikuwa iahirishwe lakini staa huyo akaomba itolewe kwa kuwa alitaka kusafiri.
Ilisemekana kuwa mbali na kuwa na safari pia aliomba itolewe kwa sababu yupo ‘bize’ na maandalizi ya arobaini ya baba yake, Isaac Sepetu aliyeaga dunia hivi karibuni.
Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe, Dar ambako ndiko kesi hiyo ilipokuwa ikirindima tangu mwezi Agosti, mwaka huu.
Wema Sepetu na rafiki zake wakijadiliana jambo eneo la Mahakama ya Mwanzo ya Kawe, Dar.
ASUBIRIWA KUPELEKWA GEREZANI, ACHOMOA ‘MADOLARI’
Ilielezwa kuwa katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa takriban saa mbili, Wema alikuwa akisubiriwa nje tayari kupelekwa gerezani lakini kama kawaida yake fedha iliongea ambapo alizamisha mkono laini kwenye ule mkoba wake na kuchomoa ‘madolari’.
Chanzo kilidai kuwa zilihitajika fedha za Kibongo hivyo Wema alichambua mkoba wake na kutoa ‘wekundu’ kumi huku akirejesha zile dola za Kimarekani.
“Wema alifanya kama alivyomfanyia Kajala siku ile pale Kisutu. Kwa Wema ishu ya fedha siyo tatizo sana. Kuliko kumpotezea muda, Wema yupo tayari kutoa kiasi chochote cha fedha.
“Kwa Wema muda ni kitu cha muhimu zaidi kuliko hata hiyo fedha ndiyo maana alitoa tu hiyo faini mara moja,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupokea maelezo hayo, gazeti hili lilimsaka Wema ili kupata mzani wa habari hiyo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Wema na shosti wake Kajala wakitoka mahakamani hapo.
Hata hivyo, alipotafutwa meneja wake, Martin Kadinda na kuulizwa juu ya suala hilo alifunguka:
“Ile kesi iliisha tangu Ijumaa iliyopita, watu hawakujua tu. Wema alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu au faini ya shilingi laki moja.
“Alichokifanya Wema alilipa faini hiyo na sasa yupo freshi na mishe zinaendelea. Unajua haruhusiwi kufanya mahojiano hadi amalize arobaini ya baba yake.”
Chanzo kilisema kuwa kabla ya hukumu hiyo, Wema alikuwa katika hali kama ile iliyomkuta Kajala wakati wa hukumu yake miezi kadhaa iliyopita kwani alikuwa akilia, kujuta na kumuomba Mola amuepushe na balaa hilo lililosababishwa na kuwa ‘tilalila’.
Hata hivyo, hukumu hiyo iliwashangaza watu kwani iliendeshwa kwa muda mrefu na kwa mbwembwe nyingi lakini hokumu yake ikawa ya kawaida tofauti na matarajio ya wengi.
Wema Sepetu na kampani yake wakiondoka eneo la mahakama.
KAJALA NAYE KICHEKO TENA
Wakati Wema akikenua, wiki hii Kajala naye ilikuwa chereko chereko baada ya Mahakama ya Rufaa Kanda ya Dar kuridhika na hukumu yake iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema mwaka huu kufuatia rufaa iliyokatwa na mume wa staa huyo Faraji Chambo.
Katika kesi ya awali, Kajala alihukumiwa kifungo cha miaka mitano au faini ya Sh. milioni 13 baada ya kupatikana na hatia ya kushirikiana na mumewe kwenye msala wa kutakatisha fedha haramu wakati mwanaume huyo akifanya kazi Benki ya NBC, Dar.
Hata hivyo, Wema alimlipia faini hiyo kama alivyofanya kwenye kesi yake.
Katika hukumu ya rufaa hiyo, majaji walijiridhisha kwamba kesi hiyo iliendeshwa ipasavyo na Kajala alitimiza taratibu za kuwa huru kwa kulipa faini lakini mumewe aliyehukumiwa miaka saba alishindwa kulipa faini ya Sh. milioni 213.
MAOMBI YAO YASIKIKA
Wema na Kajala wamekuwa kwenye maombi ya kufunga wakisali na kufanya dua ili kuwaepusha na kifungo hivyo kwa sasa wote ni vicheko.
GPL