KHADIJA KOPA AFUNGUKA KUHUSU MIDUME KUMZENGEA KILA UCHAO...

Khadija Kopa

MALKIA wa Mipasho Bongo, Khadija Omar Kopa amefunguka kuwa, tangu atoke eda amekuwa akisumbuliwa na wanaume wengi wakitaka kumuoa licha ya yeye kutokuwa na mawazo hayo kwa sasa.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar, Khadija alisema kiukweli mawazo ya kumtafuta mrithi wa marehemu mume wake, Jafari Ally, hayapo kwa sasa ila amekuwa akipokea simu nyingi na meseji kibao za wanaume wanaoomba nafasi.

 “Kwa kweli sina mawazo ya kuolewa kwa sasa lakini ni kweli nimekuwa nikipata usumbufu mkubwa sana kutokwa kwa wanaume wanaotaka ndoa na mimi. 
 “Siwezi kusema sitaolewa milele kwani Mungu ana mipango yake ila mara nyingi ninapofikiria kuolewa tena nahisi mwanaume nitakayempata anaweza kuniumiza na kunifanya nimkumbuke marehemu mume wangu,” alisema Khadija Kopa.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...