Mkalimani
wa alama za viziwi katika hafla ya kumbukumbu ya Mandela iliyofanyika
Jumanne wiki hii (Dec 10) afahamika. Anaitwa Thamsanqa Jantjie, 34.
Mkalimani huyo ameomba radhi kwa kile kilichotokea baada ya kushtukiwa
kuwa ishara alizokuwa anazitoa wakati wa hotuba za viongozi hazikuwa na
maana yoyote bali alikuwa anarusha mikono tu.
Kwa
mujibu wa Mail Online, Jantjie (34) amesema anaiweza vizuri kazi hiyo
lakini siku ya kumbukumbu ya Mandela alianza kusikia makelele kichwani
kwake yaliyosababisha aanze kutoa ishara zisizo na maana wakati wa hafla
hiyo.
Mr
Jantjie ameomba radhi kwa tukio hilo na kuongeza kuwa hakujua
kilichosababisha hali hiyo imtokee,lakini amekiri kuwahi kulazwa
hospitali ya vichaa kwa zaidi ya mwaka mmoja.
“’There
was nothing I could do. I was alone in a very dangerous situation. I
tried to control myself and not show the world what was going on. I am
very sorry. It’s the situation I found myself in.” Mr Jantjie aliliambia
gazeti la Star newspaper la Johannesburg.
Aliongeza
kuwa “What happened that day, I see angels come to the stadium … I
start realizing that the problem is here. And the problem, I don’t know
the attack of this problem, how will it comes. Sometimes I react violent
on that place. Sometimes I will see things that chase me,”.
Jantjie akizunguzma nyumbani kwake Bramfischerville, South Africa, jana (Dec. 11, 2013)
Ameongeza
kuwa licha ya kujigundua alikuwa kwenye hali ngumu, lakini alijitahidi
asipanic kutokana na ulinzi mkubwa uliokuwa umemzunguka, kwasababu
hakutaka kuiaibisha nchi yake.
Mkalimani
huyo amedai kwamba alifanya kazi na kampuni iitwayo SA Interpreters
iliyopewa kazi na ANC kwa ajili ya hafla ya kumbukumbu ya Mandela,
iliyohudhuriwa na viongozi wa mataifa mbalimbali akiwezmo Rais wa
Marekani Barrack Obama katika uwanja wa FNB, Johannesburg Jumanne wiki
hii.
Shirika
la habari la AP lilipojaribu kumuonesha video clip ya tukio hilo wakati
anatafsiri katika memorial service ya Mandela, Jantjie alisema
hakumbuki chochote alichooneshwa katika video hiyo licha ya kuwa ni yeye
aliyekuwa anakalimani,”I don’t remember any of this at all”, alisema.
Mr
Jantjie amesema alilipwa dola 85 (135,000 Tsh) kwaajili ya kukalimani
siku hiyo. Mr Jantjie amedai kuwa ukalimani ndiyo kazi yake ya kila
siku inayomuingizia kipato.
SOURCE: MAIL ONLINE