Akizungumza na Amani, mke wa Nelson aliyejitambulisha kwa jina la Neema Hamis Zame (32), alikuwa na haya ya kusema:
“Siku ya tukio, ilikuwa alfajiri kabla hatujaamka, ghafla nilimsikia shemeji yangu aitwaye Goodluck (Ainea Shoo) akipiga kelele na kusema: ‘Kaka kuna mwizi.’ Mume wangu aliamka akatoka kuelekea sebuleni na mimi nilikuwa nyuma yake.
“Kufika,
tulimkuta shemeji amelala sakafuni huku utumbo ukiwa nje na damu nyingi
zikimtoka, alikuwa akikoroma, kumbe alichomwa kisu kwenye paja, mara
mbili tumboni na begani.
“Nilikimbilia chumbani kuchukua khanga na kumfunga ili kuzuia damu
isitoke kwa wingi, pia utumbo usiendelee kumwagika huku mume wangu
akimdhibiti yule mtu.
“Cha ajabu, muda mfupi mume wangu naye akawa chini anatokwa damu,
kumbe hata yeye alikuwa amechomwa kisu mara tatu tumboni na utumbo
ukatoka nje.
“Hali ndani ilikuwa mbaya, sakafu ilitapakaa damu. Nikamwita shemeji yangu mwingine aitwaye Erick (Ainea Shoo), yeye akapambana na yule mtu wakati mimi nawahudumia wale majeruhi.
“Nilipata
akili za haraka, nilikwenda kumuita mlinzi akaingia na kushirikiana na
shemeji wakamdhibiti. Huwezi kuamini, eti yule mtu akaomba asamehewe kwa
vile hakujua kama alikuwa ameingia katika nyumba yetu.
“Hakuna aliyemsikiliza kwani alikuwa amefanya kosa kubwa, akaingizwa kwenye gari hadi polisi kuchukua PF3 na likafunguliwa jalada (OB/RB/20201/2013 Kujeruhi) kisha majeruhi tukawapeleka Hospitali ya Muhimbili. “Kilichotokea hospitali, shemeji alitolewa bandama kwa vile iliharibika kutokana na majeraha ya kisu,” alisema Neema.
Naye baba mzazi wa majeruhi hao, mzee Ainea Shoo ambaye alitoka Machame Moshi, Kilimanjaro baada ya kupata taarifa hizo, alisema mtuhumiwa huyo alikuwa na dhamira ya kuwatoa roho watoto wake hao, akaliomba jeshi la polisi kushughulikia kesi hiyo kwa uwazi na kuhakikisha haki inatendeka.
Mlinzi
wa nyumba hiyo, Boli Mtumwa alipohojiwa na gazeti hili alikiri kutokea
kwa tukio hilo na kusema yeye na mdogo wa Nelson ndiyo waliomdhibiti
mtuhumiwa na kumpeleka polisi.
Dada wa mtuhumiwa aliyejitambulisha kwa jina la Taji Mbaraka alikiri
kukamatwa kwa kaka yake huyo lakini hakuwa tayari kuzungumza zaidi kwa
sababu suala hilo lipo mkononi mwa dola.
Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Polisi Kinondoni, ACP Yusuf Mrefu alikiri
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa
huku upelelezi ukiendelea.
-GPL