TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kata 27 nchini ambazo zipo wazi
kutokana na madiwani wake kufariki dunia na wengine kupoteza sifa,
uchaguzi wake utafanyika Februari 9 mwakani. Akizungumza na Tanzania
Daima jana, Mkurugenzi wa NEC, Julius Mallaba, alisema uchaguzi huo
utafanyika katika halmashauri 23 baada ya kukamilisha taratibu
zinazotakiwa.
Alizitaja kata hizo na halmashauri zake zikiwa kwenye mabano ni Segela na Mpwayungu (Chamwino), Ukumbi na Ibumu (Kilolo), Nduli (Iringa), Malindo (Rungwe) na Santilya (Mbeya).
Nyingine ni Tungi (Morogoro), Mkwiti (Tandahimba), Mkongolo (Kigoma), Sombetini (Arusha), Mrijo (Chemba), Magomeni na Kibindu (Bagamoyo), Mtae (Lushoto), Ubagwe (Ushetu) na Namikago (Nachingwea).
Kata nyingine ni Partimbo na Loolera (Kiteto), Kiwalala (Lindi), Kilelema (Buhigwe), Kiomoni (Tanga), Kasanga (Kalambo), Rudewa (Kilosa), Kiborloni (Moshi), Njombe Mjini (Njombe) na Nyasura (Bunda).
Alisema uteuzi wa wagombea udiwani utafanyika Januari 15, wakati kampeni za uchaguzi zitaanza Januari 16 hadi Februari 8 na siku ya kupiga kura itakuwa Februari 9.