Akizungumza wikiendi iliyopita katika Viwanja vya TCC Chang’ombe jijini
Dar es Salaam ambapo kulikuwa na mechi kati ya wasanii wa Bongo Fleva na
Bongo Muvi, Ray aliwashangaa waandishi kwa kumshambulia kutoka
kimapenzi na Chuchu.
Mwandishi alianza kwa kumwuliza: “Ray magazeti yanaandika kuhusu wewe
kutoka na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtu. Mainda amezungumza mengi.
Kukaa kwako kimya bila kufafanua chochote siyo kitu kizuri. Tafadhali,
hebu zungumza japo kidogo kuhusu madai ya Mainda.”
RAY: Sikia
nikuambie, huyo Mainda utoto unamsumbua. Haniumizi kichwa kabisa. Kuhusu
Chuchu... si mmeshaandika? Endeleeni kuandika lakini soon mtashuhudia
kitu kikubwa sana.
RISASI: Ni kitu gani hicho?
RAY: Niacheni
na Chuchu wangu.... kifupi ndiye mke wangu na itawashangaza wengi.
Halafu mimi nawashangaa sana. Yaani mimi kutoka na Chuchu mnakuzaaaa...
mbona alivyokuwa na ma-boyfriend zake wengine hamkuandika? Kwa sababu ni
Ray basi mkaona ni habari. Mimi ninavyojua Chuchu siyo mke wa mtu.
Kwanza
mimi sijamchukua kutoka mikononi mwa mumewe kama mnavyosema. Chuchu
tayari alikuwa na maisha yake mapya. Nilimchukua kutoka kwa Libert
(hajafafanua zaidi ni nani). Mbona alivyokuwa na huyo Libert
hamkuandika? Kifupi niacheni na maisha yangu.
RISASI: Vipi kuhusu Johari?
RAY: (Huku akikimbia kuingia uwanjani) Tena huyo mama yako (akimuonesha mwandishi Johari) anakuja.
Mwandishi
wetu aliachana na Ray aliyekuwa akiingia uwanjani na kumfuata Johari
lakini hakuwa tayari kusema chochote achilia mbali hata kumsikiliza
mwandishi wetu!
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni gazeti hili
liliandika habari yenye kichwa MAINDA: NIMETOA MIMBA YA RAY. Ndani yake
Mainda alifunguka mengi ikiwemo kuchanganywa kimapenzi na Ray, yeye na
wenzake Johari na Chuchu Hans.
CREDIT:GPL