Ilikuwa
ni mida ya saa nane mchana ambapo Pantoni kubwa ya Mv. Magogoni ikiwa
imesheheni abiria ikiwavusha kutokea Posta kuelekea Kigamboni , ilipatwa
na wakati mgumu baada ya kushindwa kutia nanga ili iweze kusimama na
abiria waweze kushuka..
Tukio
hilo ambalo chanzo chake kimetokana na Injini za Pantoni hilo kushindwa
kufanya kazi haikuweza kutia nanga kwa muda wote huo.. na ambapo
kulikuwa na upepo mkali sana ambao ulisababisha Pantoni hiyo kukosa
muelekeo na kuanza kuambaa ambaa mpaka maeneo ya Chuo Kikuu cha Mwalimu
Nyerere kisha kusukumwa zaidi hadi eneo la bandari ya Zanzibar.
Hata hivyo baada ya hali kuzidikuwa si nzuri walilazimika kuita meli ndogo za uokoaji ambapo meli ya kwanza haikuweza kuvuta pantoni hiyo na kulazimika kuongeza meli nyingine ili iweze kuongeza nguvu pamoja na boti za Jeshi la polisi ambazo zote zilifika na kwa ushirikiano mkubwa ziliweza kufanikiwa zoezi hilo la kuirudisha pantoni hiyo katika eneo lake husika.

Na abiria ambao walinusurika kuweza kushuka na kuendelea na shughuli zao za kawaida..
Baadhi ya Abiria katika Pantoni ya Mv. Magogoni wakiwa wanatazama jinsi kivuko hicho kinavyo pepea pepea
Abiria wakiwa wamevaa mavazi maalumu ya kujiokoa na kujiweka sawa kama kungetokea hatari yoyote
Kilammoja na life jacket lake.
Kila mmoja alikuwa na wasisi wasi
Wengine walionekana kusimama kwa woga .. Wengine walionekana kuwa na wasiwasi waliamua wakae tuu chini.
Ilikuwa
ni baada ya kuanza kuvutwa na Meli zengine kuelekea katika eneo la
kushukia, ambapo kila mtu alikua anaonekana mwenye nyuso ya furaha
kuashiria kuokoka katika hatari.
Pantoni ya Mv. Magogoni ikiwa imetulia sasa na abiria wakiwa wanajiandaa kushuka huku wengine.
Picha zote na Dar es salaam yetu Blog