Baadhi ya wananchi waliofika muda wa saa 11 jioni wakielekea kwenye treni la Mwakyembe. Hii imetokana na kutokea kwa hitilafu kwenye ingini ya treni hiyo. Tatizo hilo limepelekea usumbufu kwa abiria waliofika saa 10 na wengine kufika saa 9 lakini hakuna ufumbuzi uliotolewa kuhusu tatizo ilo.
Baadhi ya abiria wakiwa wamepumzika baada ya kukaa kwenye treni la Mwakyembe kwa muda mrefu. Abiria
wanaotumia usafiri wa treni jijini Dar wamekwama kwa takribani saa tatu
sasa kwenye stesheni ya Posta. Chanzo cha kutoondoka kwa treni hiyo
inasemekana ni hitilafu kwenye moja ya vichwa vya treni hiyo hivyo
kusababisha kutoondoka kituoni hapo. Abiria wengi wamekwama na
wanalalamika bila kupata majibu ya uhakika kutoka kwa uongozi wa TRL.
(PICHA NA PAMOJAH PURE BLOG)