Watu waliokimbia makaazi yao kutokana na vita nchini Sudan Kusini, wakisubiri maboti kuvuka mto Nile, katika mji wa Bor. |
Mapigano yanaendelea nchini
Sudan Kusini licha ya pande mbili zinazohusishwa na mgogoro wa nchi hiyo
kujiandaa kwa mazungumzo ya amani nchini Ethiopia.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini ameiambia BBC
kuwa mapigano yanaendelea katika mji wa Bor na baadhi ya sehemu za jimbo
la Unity.
Pande zote mbili za serikali na
waasi wamepeleka wajumbe wao katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Mpaka sasa waasi wamekataa kusitisha mapigano, wakati mazungumzo ya
kutafuta suluhisho la mgogoro huo yakiendelea.
Mashirika ya misaada yamesema msaada wa dharura unahitajika haraka kwa maelfu ya watu waliolazimika kuyakimbia makaazi yao.
Hali imezidi kuwa mbaya katika kambi ya
wakimbizi ya Awerial iliyopo katika kingo za mto Nile- ambako sasa ni
makaazi ya watu 75,000 waliokimbia mapigano jirani na Bor, mji mkuu wa
jimbo la Jonglei, ambalo kwa sasa linadhibitiwa na waasi. Mji wa Bor
umekuwa ukibadilishwa udhibiti wake kati ya majeshi ya serikali na
waasi, kutokana na umuhimu wake. Mara ya kwanza ulitwaliwa na waasi,
lakini ukakombolewa na majeshi ya serikali na sasa umerudi tena mikononi
mwa waasi.
"Hakuna maji safi ya kunywa. Visima vitano- havitoshi," David Nash wa shirika la madaktari wa MSF ameiambia BBC.
"watu wanakunywa maji moja kwa moja kutoka mto
Nile. Yna matope, si mazuri. Na hakuna vyoo, kwa hiyo magonjwa ya
kuambukiza yanajitokeza. Kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kama
kipindupindu, ni hali inayowezekana kabisa kutokea.
BBC