Home »
Uncategories »
ALIYEZAA NA SHILOLE AIBUKA, WAONYESHANA MAHABA HADHARANI LAIVU
ALIYEZAA NA SHILOLE AIBUKA, WAONYESHANA MAHABA HADHARANI LAIVU
Unknown
10:36 AM
Denis Mtima, aliyekuwa Igunga, Tabora
KWA mara ya kwanza, mzazi mwenza na msanii wa muziki na filamu Bongo,
Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Elias Makala ameibuka na kujinadi hadharani
wilayani Igunga, Tabora.
Shilole akiwa na mzazi mwenzake Elias Makala.
Tukio hilo lilitokea Februari 14, mwaka huu (Valentine’s Day) ambapo
Shilole aliyekuwa amekwenda kufanya shoo mkoani humo, alishindwa kuzuia
hisia zake baada ya mzazi mwenzake huyo kujitokeza na kujikuta
wakioneshana mahaba mbele za watu.
Pozi
hilo la kimahaba liliwashangaza watu na kuanza kudhani kuwa huenda
wawili hao wakarudisha penzi lao lililokufa miaka mingi iliyopita.
“Mh!
Kweli mtalaka hatongozwi, hebu ona Shilole alivyorembua alipomuona
jamaa yake, pale Makala kumchukua ni kama kumsukuma mlevi,” alisema
shuhuda mmoja.
Shilole akiwa na mzazi mwenzake klabu.
Baada ya paparazi wetu ‘kuusoma mchezo’ huo, aliamua kumuuliza staa huyo kama penzi lao limerudi upya au laa?
“Hahahahaa! Kwa kweli unanichekesha kuniuliza kama nimerudisha penzi
kwa mzazi mwenzangu, huyu ni baba wa mwanangu Joyce, itabaki kuwa hivyo.
Siwezi kumtenga na sioni ajabu kupiga naye picha, hakuna
kinachoendelea,’’ alisema Shilole.
Licha ya kufafanua hivyo, usiku wa siku hiyo, Shilole alipokuwa
jukwaani akipagawisha mashabiki kwa shoo kali, alimpandisha jukwaani
mzazi mwenziye huyo hali iliyozua mtafaruku mkubwa kwa mpenzi wa sasa wa
Makala aliyefahamika kwa jina la Maguno.
Baada ya shoo kuisha, Maguno aliyekuwa na jazba kwa mpenzi wake
kupandishwa jukwaani, alimsaka Shilole kwa udi na uvumba kutaka
kumtembezea kichapo lakini bahati haikuwa yake, hakuweza kumpata hadi
msanii huyo aliporejea jijini Dar siku iliyofuata.