
MWANADADA mtangazaji na mjasiriamali, Maimartha Jesse anaonekana kuukaribisha upofu kufuatia kukithiri kutumia gundi katika kujipachika kope bandia.

Katika tukio la hivi karibuni mwanadada huyo alionekana akiwa amejibandika gundi katika harakati ya kujibandika kope hizo na alipoulizwa na paparazi wetu kama haogopi madhara yake alisema:
“Huo ni urembo tu, nimebandika hivyo nikiwa katika maandalizi ya kubandika kope katika macho yangu, sidhani kama naweza kupata tatizo lolote.”