Baadhi ya mastaa wakionyeshana ufundi wa kucheza.
...Ilikuwa ni full kukata mauno ndani ya Letasi Lounge.
...Burudani baada ya kukolea, hali ilikuwa hivi.
Husna Maulid akionyesha ufundi.
“Duh! Yaani utafikiri watu hawajui kuwa hii
ni Kwaresma, ni full laana hebu angalia Husna Maulid, Sajent (Husna
Idd) na Davina (Halima Yahya) wakiongozwa na Muna wanavyojichetua hadi
‘makufuli’ yanaonekana,” alisema mwanadada mmoja.
Husna Idd 'Sajent' naye akionyesha machejo yake.
Katika hatua nyingine, mwanaume tata
anayejulikana kwa jina la Agrey alivua nguo na kubaki na ‘kufuli’ kisha
alipanda juu ya kiti na kuanza kuonesha staili mbalimbali za ukataji wa
mauno.
“Tobaa… jamani mwangalieni Agrey, kavua nguo anamwaga radhi…hahahaaa,” alisikika msanii mmoja wa Kundi la Vituko Show.
...Sajent na Husna wakizidi kujiachia.Ili kunusuru hali, mshereheshaji wa shughuli hiyo, Chumi Suleiman ‘Bi Hindu’ alilazimika kuzima muziki kuepusha laana iliyokuwa inazidi kuvuka mipaka.
“Jamani
hata mimi nina watoto wa kiume na kike, sasa hii hali siwezi
kuivumilia, nazima muziki na shughuli ndiyo imemalizika maana wote humu
ndani tutaonekana siyo,” alisema Bi Hindu ambapo baada ya kusema tu,
aliambulia mvua ya matusi.
