Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na dada yake wa hiyari, Halima Kimwana.
Halima Kimwana alielezea sakata hilo wikiendi iliyopita baada ya
kuulizwa undani wa skendo inayomkabili ya kumkuwadia au kumtongozea
Diamond kwa mastaa na kuwabadilisha kama nguo.Kwa mujibu wa Halima Kimwana, huwa Diamond hajisumbui kumtongoza mwanamke zaidi ya hao mastaa kujitongozesha wenyewe kwake.
Halima na Diamond katika pozi.
Halima Kimwana alidai kwamba yeye kama dada wa mwanamuziki huyo
(hakutaka kufafanua dada kivipi), amefikia hatua ya kusumbuliwa na
wasichana wa kila aina hasa mastaa wakimuomba awatongozee kwa Diamond
tena kwa ahadi kemkemu.“Kwani unafikiri Diamond anajihangaisha kuwatongoza hao mastaa? Wao ndiyo kila kukicha wanamsumbua na kutuhangaisha sisi wakitaka tuwatongozee kwa kaka yetu.