Mafundi
wa Kampuni ya Oilcom wakiangalia mabaki ya lori la kampuni hiyo
lililochanika baada ya kulipuka kwa tanki lake wakati likichomewa katika
eneo la Tabata Relini, jijini Dar es Salaam jana. PIcha na Emmanuel
Herman
Taharuki
ya aina yake ilitokea jana eneo la Tabata Relini kwenye yadi ya malori
ya Kampuni ya Oilcom baada ya kutokea kishindo kikubwa kilichotokana na
kupasuka kwa tanki la mafuta
Tukio
hilo lililotokea saa 11 jioni, lilizua hofu miongoni mwa wakazi na
wafanyakazi wa eneo hilo, na lilitokana na hitilafu ya kiufundi wakati
wa kulitengeneza tanki hilo.
Mashuhuda
wa tukio hilo lililojeruhi watu watatu waliliambia Mwananchi kuwa
mlipuko huo ulitokea wakati fundi akichomea sehemu ya tanki katika
karakana ya magari ya kampuni hiyo.