Sunday Demonte (Picha hii ni ya akaunti yake ya facebook)
Sunday Demonte akiwa na mkewe Aunt Ezekiel wakati wa harusi yao huko Dubai mwaka 2012
Hapa Sunday na Aunt Ezekiel wakiwa na mtoto wa mmoja wa marafiki zao huko Dubai
Habari ambazo zimetufikia hivi punde ni kwamba yule shemeji wa wana
Bongo Movie na walimbwende hapa nchini Papaa Sunday Demonte ambaye
alimuoa Aunt Ezekiel yupo sero hivi sasa katika moja ya viunga vya dola
vya Dubai. Taarifa hii kutoka chanzo chetu cha uhakika cha karibu na
Pendeshee huyu wa magari kutoka huko Dubai zinasema Pendeshee huyu
amekamatwa kwa madai mbalimbali likiwemo la kuto kuishi kihalali katika
Nchi hiyo kwa kipindi kirefu ambayo ni maarufu kwa biashara duniani.
Kwa mujibu wa chanzo chetu Papaa huyu alikuwa akisakwa muda mrefu sana,
ata wakati anafunga ndoa na Aunt Ezekiel alikuwa akiishi kimashaka
mashaka kwa kuogopa kuingia katika mikono ya dola ya waarabu hao. Papaa
huyu mwenye kupenda kuwa na mabinti wa kitanzania ambao ni maarufu,
chanzo kilienda mbali zaidi na kututanabaisha ya kuwa pia amewahi kuwa
na mahusiano na baadhi ya wasanii wa kike waliowahi kukata nyonga katika
moja ya bendi maarufu hapa jijini Dar es salaam. Mtandao huu
umejitahidi kumtafuta Aunt Ezekiel ili kumuuliza kama taarifa hizi
anazo, ila simu yake haikupatikana mpaka tunaingia mitamboni, vile vile
mtandao wako unajaribu kuwasiliana na mwakilishi wetu wa serikali nchini
humo Bwana Omary Mjenga ili kuweza kujua kama wana taarifa yoyote ya
kukamatwa kwa mtanzania huyu na nini wanatakiwa kufanya ili kuweza kujua
chanzo kikuu na nini hatua ambazo zinatakiwa kufuatwa za kuweza
kumsaidia.
Taarifa zaidi tutawajulisha pindi tutakapowapata watu wengine ambao
tunawatafuta ili kuweza kujua ni nini cha kufanya ili kumuwezesha atoke
na kuweza kuishi salama salmin.