Kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jana, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, #Ahmed Kipozi, alifika eneo hilo na kujionea wananchi wakitaabika kuvuka katika eneo hilo na huku magari ya abiria yaliyokuwa yakitokea Bagamoyo kwenda Kiwangwa, yakibeba abiria na kuishia eneo hilo na kubeba wengine walioshushwa upande wa pili na kugeuza kwa kila abiria kulipa Sh. 1000. Na kisha abiria hao wakipata usafiri mwingine wa kubebwa na Vijana waliopo eneo hilo kwa Sh. 2000 kwa aliyependa ama 500 kwa kuongozwa njia.


''WA HUKU WA HUKU NA WA HUKO WA HUKO''
Baada
ya hapo Mkuu huyo wa Wilaya alitoa tamko na kuwataka wakazi wa Kiwangwa
kutokwenda Bagamoyo na waBagamoyo kutokwenda Kiwangwa, kwa kipindi
chote cha mvua ili kuepuka maafa yanayoweza kutokea kwa kutumbukia na
kusombwa na maji, ama daraja hilo la Jeshi kukatika kutokana na maji
kuanza kupita juu ya daraja hilo jana.
Mkuu
wa Wilaya, akizungumza na madereva wa magari waliokuwa wakisubiri
kuvuka eneo hilo pamoja na vijana waliokuwa wakitoa huduma ya kuwavusha
watu.
Vijana wakifanya kazi yao ya kuwavusha watu eneo hilo.
Baadhi ya magari yaliyokaidi amri yakivuka eneo hilo.
Vijana
hao waliwavusha hadi wagonjwa katika eneo hilo kama anavyoonekana
pichani akiwa amembeba mtu mzima anayeonekana kuwa ni mgonjwa.
Baadhi ya vijana walijiona kama wapo Beach, walikuwa wakipiga mbizi na kuogelea eneo hilo kwa furaha.
Magari yakiwa katika foleni kusubiri kuvuka eneo hilo.
Baadhi
ya abiria walioshushwa upande wa pili wakiwania usafiri wa kuelekea
Bagamoyo baada ya kufaulishwa na gari jingine la uapnde wa pili.
Hawa nao ni wa upande wa pili
Gari la Abbas Tarimba likivuka eneo hilo.
Vijana wakijipigia debe kwa dereva ili akibali kuvushwa, bila kujua kuwa ndani yake alikuwapo Mkuu wa Wilaya hiyo.
Katapila lililoletwa ili kuziba eneo hilo kuzuia magari kuvuka....

















>>Sufiani Mafoto.com