Stori: Gladness Mallya
STAA wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amekiri kubebeshwa
madawa ya kulevya bila kujua na kujikuta akiponea chupuchupu kutokana na
umaarufu wake.
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akizungumza na paparazi wetu, Dude alisema amewahi kubebeshwa unga na
rafiki yake wa karibu ambaye hakumtaja jina na walikuwa wakitokea
Nairobi nchini Kenya kuja Tanzania.Alisema wakati wanaanza safari
alipewa koti la baridi na rafiki yake huyo, akalivaa kumbe ndani yake
lilikuwa limeshonewa pakti za unga.
Walisafiri kwa gari na kila walipokutana na polisi wanaokagua
hawakumkagua Dude kwani waliishia kupiga naye picha na kumsifia kwa kazi
yake mpaka alipofika jijini Dar es Salaam.
“Kila tulipokuwa tunakutana na polisi rafiki yangu alikuwa akiwawahi
na kuwaambia kwamba yupo na mimi ambapo walifurahia kuniona na kupiga
picha na mimi bila kunikagua chochote,” alisema
Dude.
Dude.
Baada ya kupita vizingiti vyote, waliingia jijini Dar es Salaam
maeneo ya Kinondoni Manyanya alipokuwa akiishi rafiki yake huyo ambapo
alimwambia avue koti, akaanza kufungua mzigo aliokuwa ameushonea kwa
ndani.
Dude alijikuta akishikwa na tumbo la kuhara kutokana na mshtuko
alioupata baada ya kuona rafiki yake huyo akitoa madawa ya kulevya.
“Jamaa alinipa shilingi elfu hamsini za Kenya na ni baada ya kufika
Dar ndipo niligundua kwamba nilikuwa nimebebeshwa unga lakini yule jamaa
alishakamatwa na anatumikia kifungo nchini Pakistani,” alisema Dude.
Hata hivyo Dude aliwashauri mastaa wenzake kuwa makini na marafiki
zao kwani siyo wote wanaokamatwa wamebeba unga kwa kujua bali wengine
wanabebeshwa tu bila kujua.