Mtu
mmoja amefariki dunia na 19 wamejeruhiwa na kuporwa vitu mbalimbali
zikiwemo simu za mkononi na fedha baada ya majambazi kufunga barabara
kwa mawe na magogo na kisha kuteka magari katika eneo la mkata doma
barabara ya morogoro iringa.
Kwa
mujibu wa kaimu kamanda polisi mkoa wa Morogoro John Laswai amesema
tukio hilo limetokea majira ya usiku ambapo majambazi hao wakiwa na
silaha mbalimbali waliteka magari na kujeruhi abiria ambapo aliefariki
dunia amefahamika kwa jina la Richard Mgombea ambaye alifariki wakati
akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Morogoro na magari ya
magazeti ya kampuni ya Mwananchi limetumbukia mtoni wakati wakijaribu
kukimbia majambazi hao. Nao
majeruhi waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro wakielezea
tukio hilo wamesema wao ni madareva wa magari ya it na walikua
wakitokea Mbeya kurudi Dar es salaam wakikutana na foleni kubwa
barabarani ndipo wakatekwa na kujeruhiwa ambapo wamekiri kupoteza fedha
mali na simu za mkononi.
Nae
mganga wa zamu katika hospitali ya mkoa wa Morogoro Dr Erick Rwegoshora
amekiri kuwepo kwa taarifa za kifo na wamepokea majeruhi wengine
wamelazwa na wengine walitibiwa na kuruhusiwa .
CHANZO: ITV