Mshambuliaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor (kushoto) akifunga bao la kwanza la kusawazisha na kufanya ubao usomeke 1-1
Mpira kambani: Mlinda mlango wa Sunderland Vito Mannone (kulia) akiushangaa mpira uliozamishwa nyavuni na Adebayor
Heshima: Kocha wa SpursTim Sherwood (kulia) akimpigia saluti Adebayor baada ya kufunga bao la pili.
TOTTENHAM imeishushia kipigo kizito cha mabao 5-1 klabu ya Sunderland katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England usiku huu.
Kocha
mkuu wa Spurs, Tim Sherwood amebaki ameduwaa baada ya vijana wake
kuonesha soka safi wakati yeye yuko mbioni kuondolewa katika wadhifa
huo.
Spurs
tayari wameshatangaza kuwa mwishoni mwa msimu Sherwood hataendelea kuwa
kocha mkuu, badala yake wanamhitaji Van Gaal ambaye ni kocha wa timu ya
Taifa ya Uholanzi.
Mabosi wa Spurs wanataka kukifanyia maboresho makubwa kikosi chao majira ya kiangazi mwaka huu.
Shukurani
zimwendee mshambuliaji raia wa Togo, Emmanuel Adebayor aliyefunga
mabao mawili, huku mengine yakitiwa kambani na Harry Kane, Christian
Eriksen na Gylfi Sigurdsson.
Baada ya matokeo ya mechi zote wikiendi iliyopita na leo usiku, timu kumi bora katika msimamo hizi hapa chini;