Picha na maktaba |
Imetokea usiku wa kuamkia leo ajali mbaya maeneo ya Ikungi, Singida ikilihusisha basi la Sumry linalosafiri kati ya Kigoma-Dar.Inasemekana mwendesha baiskeli alikuwa akivuka barabara lori likamgonga ghafla wanakijiji wamejaa kushangaa tukio na askari akipima ajali ndipo likatokea basi la Sumry na kugonga watu kumi na tatu pamoja na askari ni wa 14 mpaka sasa ndio idadi kamili ya waliopoteza maisha.WATU 13 akiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida
Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori
lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati
wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea
kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu
hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha
eneo hilo.
Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama
eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi
Ikungi, Singida. Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo
imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi
wawili waliopelekwa hospitalini hapo.