Mmoja wa majeruhi wa mapigano hayo akiwa amelazwa hospitalini. |
Watu
wanne wamekufa na wengine tisa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya
hiyo mkoani Tabora, kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji,
yaliyotokea katika Kijiji cha Isakamaliwa wilayani Igunga.
Mkuu
wa Wilaya ya Igunga, Elibarik Kingu alitaja waliofariki ni Chawala
Doke, Mohammed Msengi, Biblo Kingu na Peter Karongo, wote wakazi wa
Kijiji cha Isakamaliwa.
Mapigano
hayo yalitokea juzi saa 7 mchana. Kingu alisema pia nyumba 12
zimechomwa moto na uharibifu mkubwa wa mali za wakazi wa kijiji hicho.
Wafugaji wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, pembezoni mwa mto Manonga, ndiyo wanatuhumiwa kufanya mauaji.
Kwa
mujibu wake, zaidi ya watu 20 hawajulikani waliko na zaidi ya watu 150
hawana makazi, kutokana na nyumba zao kuchomwa moto kwenye mapigano
hayo.
Chanzo cha mapigano ni wafugaji kulisha mifugo katika mashamba ya wakulima wilayani Igunga.
Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora na ya Mkoa wa Shinyanga,
zilifika eneo la tukio na kushuhudia uharibifu uliofanyika. Kikao hicho
kiliendelea kupata usuluhishi wa mgogoro huo na kuchukua hatua kwa
waliohusika katika mauaji na uharibifu.CHANZO NA ZIRRO BLOG