BREAKING NEWS:: SUAREZ HUENDA AKAKOSA KUCHEZA KOMBE LA DUNIA 2014 BRAZIL

Luis Suarez
Mshambuliaji wa Timu za Liverpool na Uruguay Luis Suarez sasa anaweza kufanyiwa upasuaji wa goti lake na Kuwa na shaka kubwa Kushiriki kwake katika michuano ya Kombe la Dunia Mwaka 2014, habari ambayo itakuwa ahueni kwa Kikosi cha England Cha Kocha Roy Hodgson.

Nyota huyo wa Majogoo wa London, ambaye alichaguliwa na PFA Mchezaji wa Mwaka na wenzake baada ya kufunga mabao 31 katika kikosi cha Brendan Rodgers' ambacho kilifukuzia ubingwa wa ligi ya England, Wachezaji wenzake katika Timu ya Taifa waliona baadhi usumbufu wakati wa mazoezi yake siku ya Jumanne. Na baada ya vipimo imeonyesha Hitilafu katika Misuli yake katika goti lake, Mchezaji huyo mwenye umri wa Miaka 27 anaweza kufanyiwa upasuaji wiki hii.

Amerika ya Kusini kwa upande wao wana matumaini kwamba atapona haraka na kuwa tayari kwa ajili ya mashindano hayo.

Uruguay wamewekwa katika kundi D katika Kombe la Dunia Nchini Brazil, pamoja na Uingereza, Italia na Costa Rica, habari Hii itakuwa ahueni kwa vijana wa Roy Hodgson, ambao sasa wataweza kukutana Uso kwa uso na Kikosi cha Oscar Tabarez Juni 14. Hata hivyo, Tabarez Anaweza pia kuwaita wachezaji hawa Edinson Cavani na Diego Forlan, Kuongoza Katika Upande wa Ushambuliaji ikiwa Suarez atakuwa na shaka la Kukosekana kabisa.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...