Dr. Harrison Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi akitoa ufafanuzi
wa kufukuzwa kwa wafanyakazi 13 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwl.
Nyerere.
Zaidi ya Maofisa kutoka wizara tatu wapato 13 waliokuwa
wakifanya kazi katika uwanja wa kimataifa wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere,
wamerudishwa katika wizara zao kwa kosa la kupokea rushwa kwa wageni wanaoingia
kutoka nchi mbalimbali.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam
Waziri wa Uchukuzi Dr. Herrison Mwakyembe alisema kuwa, maofisa hao walikuwa
katika kitego cha Wizara ya Kilimo, Wizara ya Afya na Wizara ya Mifugo na
Uvuvi.
Wageni ambao walikuwa wanakaguliwa na kuobwa rushwa na
wafanyakazi hao ni kutoka nchini China, India na Nchi za Kiarabu, ambao
wakifika uwanjani hapo wanakaguliwa mabegi kama amebeba dawa za asili dawa hizo
huchukuliwa na maofisa wa kilimo na baadae kuobwa pesa na kurudishiwa dawa
hizo.
Pia kama ameingia hajachoma sindano ya homa ya manjano
anaamriwa na kuulizwa kwanini hujachoma na akioneakana anakaidi anaambiwa atowe
chochote kitu kisha anaachiwa, hivyo hivyo kwa upande wa uvuvi na mifugo nako
wanafanyiwa hivyo.
Kufuatia malalamiko hayo ya wageni wanaoingia hapa nchini,
wageni hao waliamua kuyapeleka kwa Waziri Mwakyembe, naye bila ya kusita
aliunda tume ambayo iliangalia kamera za usalama na kupata maofisa 13
waliobainika kufanya uchafu huo, ambao unachafua taswira ya nchi yetu na
kuwakimbiza wawekezaji.