Stori: IMELDA MTEMA
STAA wa sinema za nyumbani (Swahili Hood), Kajala Masanja amegeuka kituko nyumbani kwa Wema Isaac Sepetu, Kijitonyama, Dar baada ya kulewa tilalila na kuwaacha midomo wazi wasanii wenzake, Ijumaa Wikienda lina kisa na mkasa.

Kajala Masanja.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Kajala alifanya madudu hayo mwishoni mwa
wiki iliyopita alipokuwa akirekodi filamu yake inayokwenda kwa jina la
Laana ambapo waigizaji wenzake walikuwa nje wakisubiri atoke aanze
‘kushuti’ kumbe alikuwa kaegemea mlango huku akiangua kicheko bila kujua
afanye nini.
Ilisemekana kuwa baada ya maji kuzidi unga, mwongozaji wa filamu
hiyo, Leah Ndemesamkye ‘Lamata” ilibidi ashikwe na kigugumizi baada ya
kuona mauzauza hayo ya Kajala na kumuuliza ni kitu gani ambacho
kimempata kwani kila anachoongea naye, yeye anaishia kucheka mfululizo.
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lilimvutia waya Kajala ili
kudhibitisha madai hayo ambapo Kajala alikiri kulewa kidogo na kumtupia
mpira rafiki yake kipenzi Wema kuwa ndiye aliyemnywesha.
Alisema: “Unajua nini, siku hiyo tulilala kwa Wema, ndiye
aliyeninywesha pombe lakini mbona kazi iliendelea kama kawaida jamani?”