Heshima za mwisho zikitolewa mbele ya jeneza lenye mwili wa Nelson Mandela 'Madiba' kabla ya maziko.
Rais
wa Afrika Kusini, Jacob Zuma (wa pili kushoto) akiwa na mjane wa
Mandela, Graca Machel (wa tatu kushoto) na mke wa zamani wa marehemu,
Winnie Madikizela-Mandela (wa kwanza kushoto) wakiwa karibu na jeneza la
Mandela kijijini Qunu kabla ya maziko.Wajukuu
wa Mandela, Ndaba (kushoto) na Mandla Mandela (katikati) wakiliangalia
jeneza wakati wa shughuli za mazishi ya Rais wa kwanza mweusi wa Afrika
Kusini.
Jeneza lenye mwili wa Mandela likisogezwa eneo la makaburi baada ya kushushwa kwenye gari tayari kwa mazishi.
Jeneza lenye mwili wa Mandela likisogezwa eneo la makaburi baada ya kushushwa kwenye gari tayari kwa mazishi.
Msafara wa kuelekea eneo la kaburi alipozikwa Hayati Nelson Mandela.
Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela enzi za uhai wake.
Nelson Mandela akiwa na mke wake wa kwanza Evelyn Mase siku ya ndoa yao mwaka 1944.
Nelson Rolihlahla Mandela akiwa na mke wake wa pili Nomzamo Winfreda Madikizela siku ya ndoa yao Juni 14, 1958.
Nelson Mandela akisherehekea kutimiza miaka 80 mwaka 1998 na ndiyo siku alipomuoa Graca Machel.
Mandela akiwa amevaa nguo za kiasili.
Helkopta tatu zilizobeba bendera za Afrika Kusini zikipita eneo alilozikwa Mandela kutoa heshima za mwisho.
Jet za Afrika Kusini zikiwa angani katika kijiji cha Qunu alipozaliwa na kuzikwa Mandela.
Mizinga 21 ya kivita ikipigwa wakati wa maziko ya Nelson Mandela Desemba 15, 2013 kijiji cha Qunu.
Mizinga 21 ya kivita ikipigwa wakati wa maziko ya Nelson Mandela Desemba 15, 2013 kijiji cha Qunu.
Mke
wa pili wa Nelson Mandela Winnie Madikizela Mandela (kulia) na mjane wa
marehemu Graca Machel (katikati) wakitembea pamoja wakati wa maziko ya
Mandela.
Askofu Desmond Tutu (katikati) akiwa na viongozi wenzake wa kidini wakati wa maziko ya Nelson Mandela.
Mjukuu wa Mandela, Mandla Mandela (kulia) akiangalia machifu wanaolisindikiza jeneza lenye mwili wa Mandela lililofunikwa na ngozi ya simba lilipowasili kijijini Qunu.

Mtoto wa Malkia wa Uingereza, Charles, akisalimiana na Mfalme wa kabila la Xhosa, Zwelonke Sigcawu wakati wa maziko ya Mandela.
Winnie Mandela (kushoto) na Graca Machel wakifuta machozi katika shughuli za mazishi ya Hayati Nelson Mandela.
Mtoto wa kike wa Hayati Mandela, Zindzi Mandela (kushoto) akimfariji mwenzake wakati wa shughuli za mazishi.
Mtoto wa kike wa Mandela, Makaziwe Mandela, akiwa jirani na kaburi la marehemu baba yake wakati wa shughuli za mazishi.
Mjukuu wa Mandela, Nand, akitoa neno wakati wa shughuli za mazishi ya babu yake.