Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba
jina la Tanzania kwa muda mrefu sasa limetawala vichwa vya habari katika
vyombo vingi vya habari duniani kutokana na Serikali kushindwa
kukomesha vitendo vya ujangili dhidi ya wanyamapori walio katika hatari
ya kutoweka, wakiwamo tembo.Tanzania sasa inaonekana mbele ya
jumuiya ya kimataifa kama taifa la watu wa ovyo, ambalo halitambui
kwamba kuangamiza wanyamapori litakuwa maskini milele.
Pamoja na kushutumiwa na kusutwa kila kona ya dunia kutokana na kushamiri kwa vitendo vya ujangili ambavyo vinasababisha mauaji ya tembo 11,000 kila mwaka, Serikali imebaki kulalama dhidi ya vyombo vya habari vya kimataifa vinavyoinyooshea kidole, ikikanusha shutuma hizo na kutishia kuvichukulia hatua za kisheria.
Wiki iliyopita, kwa mfano magazeti ya Daily Mail na Mail on Sunday ya Uingereza yalichapisha habari za kuishutumu Serikali na kudai kuwa, pamoja na kuwafahamu fika majangili wanaoteketeza wanyamapori nchini imeshindwa kabisa kuwachukulia hatua.
Katika kile kinachoonekana kwa wachambuzi wa masuala ya maliasili kama kujaribu kupoza joto la shutuma hizo, Rais Jakaya Kikwete ambaye aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kongamano hilo, juzi alifanya mahojiano jijini London na vyombo vikubwa vya utangazaji duniani, vikiwamo CNN na BBC kuhusu tatizo la ujangili nchini na juhudi za Serikali yake za kupambana na vitendo hivyo.
Wakati Rais akichukua hatua hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alikuwa tayari amefanya mazungumzo na wahariri wa magazeti ya Daily Mail na Mail on Sunday jijini London kutokana na magazeti hayo kuchapisha habari zilizoishutumu Serikali ya Tanzania kwa kutokomesha vitendo vya ujangili.
Hali hiyo ya nchi yetu kushutumiwa na kuaibishwa kwa kiwango hicho kikubwa ilichochewa na kongamano lililoitishwa na Serikali ya Uingereza na kumalizika mwishoni mwa wiki mjini London, ambapo wajumbe kutoka nchi 46 na mashirika 11 ya kimataifa yalihudhuria, wakiwamo marais wanne wa Afrika.
Katika kongamano hilo ambalo pia lilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na mtoto wa Malkia Elizabeth, Prince Charles wakuu wa nchi na wahifadhi kutoka kote duniani walibuni mikakati ya kukomesha uwindaji haramu wa wanyamapori walio katika hatari ya kuangamia.
Tanzania ndiyo iliyoonekana kuwa katikati ya masikitiko na shauku za wajumbe wa kongamano hilo kutokana na ukubwa wa tatizo la ujangili hapa nchini ambao mpaka sasa umeangamiza idadi kubwa ya faru na tembo.
Kwa sababu za kidiplomasia na kiitifaki, ujumbe wa Tanzania haukuwekwa kitimoto kwa maana ya kushinikizwa kuonyesha dhamira au kutangaza mikakati na sera mbadala za kupambana na ujangili.
Hata hivyo, Waziri Nyalandu alitangaza katika kongamano hilo kwamba Tanzania sasa imefuta mpango wake wa kutaka ipewe kibali cha kuuza shehena kubwa ya meno ya tembo yaliyohifadhiwa katika maghala hapa nchini.
Kongamano hilo ambalo ndilo lilikuwa habari kubwa ya dunia wiki hii sasa limemalizika. Bila shaka Rais Kikwete na ujumbe wake wamerudi nyumbani wakiwa wamepata somo la kutosha kuhusu umuhimu wa kupambana na ujangili pasipo kuyumba.
Kwa kuwa ameiambia dunia kwamba majangili nchini Tanzania wanafahamika, tunatarajia watatiwa mbaroni katika awamu ya pili ya ‘Operesheni Tokomeza Ujangili’, ambayo ameiahidi dunia kwamba itaanza muda wowote kuanzia sasa
-udakuspeacially