Wabunge nchini Uganda wamepitisha mswaada unaotoa adhabu kali kwa watu wanaowaambukiza wengine virusi vya HIV kwa maksudi.
Mswada huo unapendekeza adhabu ya kifungo cha
hadi miaka 10 kwa wale wanaopatikana na hatia na pia inapendekeza
wanawake wajawazito na wapenzi wao kupimwa virusi vya HIV.
"ni lazima waadhibiwe vikali kwa sababu kumuambukiza mtu HIV wakati unafahamu vyema kuwa wewe ni mwathiriwa ni uuhalifu,'' alisema mbunge huyo. Ni hatari sana kwa sababu mru huyo anaweza kuichanganya jamii na kumaliza watu.''
Lakini wafanyakazi katika sekta ya afya pamoja na mashirika ya kutetea haki za wanyonge, wamepinga vikali mswada huo, wakisema kwamba haitafanya lolote kudhibiti ongezeko la visa vya maambukizi.
Wengi wanasema kuwa mswada huo utaongeza tu unyanyapaa kwa watu wanaoishi na virusi hivyo. Pia wanasema kuwa watu watahofia kupimwa kwa hofu ya kutengwa na jamii.
Mswada wenyewe umepitishwa baada ya sheria kali inayopinga vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kupitishwa na rais Yoweri Museveni mwezi Februari. CREDITS- BBC