Njemba huyo akipokea kichapo kutoka kwa wafuasi wa Ukawa mkoani Moro.
NJEMBA mmoja amepokea kipigo kikali
kutoka kwa wafuasi wa Ukawa waliokuwa na mkutano mkoani Morogoro jioni
hii baada ya kudaiwa kuwa miongoni mwa waliomteka Mbunge Rose Kamli
wakati wa kampeni jimboni Kalenga, mkoani Iringa.
Njemba huyo ambaye hakufahamika jina
lake mara moja, aliangushiwa kipigo baada ya kuibuka na kuanza kumpiga
picha Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche. Baada ya kipigo cha
nguvu, njemba huyo alinusuriwa na polisi waliomchukua kumtoa mikononi
mwa wafuasi hao.
Mwenyekiti huyo wa Bavicha akithibitisha
kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki kumteka mbunge wao kwenye
uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa.
(PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)