WATU WATATU WAKAMATWA NA MENO 25 YA KIBOKO NA VIPANDE 8 VYA MENO YA TEMBO

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova akionesha sehemu ya  vipande 8 vya meno ya tembo vilivyodakwa huko Tabata Kisiwani jijini Dar es salaam
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova akikagua gari linalotuhumiwa kutumika
Sehemu ya mali zilizokamatwa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum limefanikiwa kukamata vipande zaidi ya ishirini (20) vinavyodhaniwa kuwa ni meno ya Tembo vilivyokuwa vimehifadhiwa nadni ya mfuko maarufu kwa jina la kiroba.
Tukio hili lilitokea tarehe 30/04/2014 katika kiwanda cha Nondo Steel Master kilichopo eneo la Mbozi Road (W) kipolisi Chang’ombe (M) kipolisi Temeke baada ya Polisi kupokea taarifa kuwa katika kiwanda hicho kuna mfuko wa kiroba wenye bidhaa hiyo umefichwa.
Baada ya taarifa hizo askari kikosi cha Upelelezi walifika kiwandani hapo na kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Kiwanda hicho aitwaye HITESH S/O PATEL walifanya upekuzi. 

Katika upekuzi huo polisi walifanikiwa kukamata vipande 25 vya meno yadhaniwayo kuwa ni ya KIBOKO vikiwa vimehifadhiwa ndani ya mfuko wa kiroba ukiwa umefichwa kwenye Roll ambayo ni Malighafi maalum ya kutengenezea nondo. 
Kwa mujibu wa taarifa ya maafisa wa wanyamapori ni kwamba kwa idadi ya vipande hivyo 25 ni sawa na VIBOKO 6 waliouawa ambapo meno ya Kiboko mmoja yana thamani ya Dolla za Kimarekani 1500 sawa na Shilingi za Kitanzania zaidi ya (Millioni Mbili Laki Nne na Sabini na Tano) Tshs.2,475,000.
 Hivyo kwa idadi ya VOBOKO sita thamani yake ni sawa na shilingi za kitanzania THS; 14,850,000/= (million kumi na nne, mia nane na hamsini elfu tu). 
Katika tukio hilo, polisi inawashikilia watu wawili ambao ni RASHID S/O ABDALLAH, Miaka 19, mwingine ni HEMED S/O JUMA @ KASIMU, Miaka 25. Washitakiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalowakabili pindi upelelezi utakapokamilika.
 Aidha katika tukio lingine mnamo tarehe 5/5/2014 huko maeneo ya Tabata Kisiwani karibu na uwanja wa Twiga Mkoa wa Kipolisi Ilala, Polisi wamefanikiwa kumkamata MUSA S/O LUCAS KIFARU akiwa naa vipande 8 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogram 13.5 ambavyo thamani yake T.Shs.49,500,000/= vikiwa vimehifadhiwa kwenye begi lenye rangi ya blue na nyeusi. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa .
 
NA LUKAZA BLOG


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...