ANNE KANSIIME KUTOA BURUDANI SIKU YA JUMAMOSI GOLDEN TULIP

Mchekeshaji Mahiri kutoka nchini Uganda,Anne Kansiime (wa pili kulia) akifafanua jambo mbele ya Wanahabari kuhusiana na burudani kubwa ya uchekeshaji atakayoionyesha kwa mashabiki wake hapo kesho Agosti 2,2014  katika ukumbi wa Golden Tulip,jijini Dar,Kulia kwake ni mchekeshaji mwingine kutoka nchini Kenya,Fred Omondi.
Mmoja wa wachekeshaji mahiri kutoka nchini Tanzania,atambulikae kwa jina la kisanii Mc Pili Pili akielezea jambo kwenye mkutano wa Wanahabari uliofanyika mapema leo jijini Dar,wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis,ambao ndio waandaaji wa Onesho hilo la vichekesho.
Baadhi ya Wanahabari walioshiriki mkutano huo wa wasanii wa vichekesho uliofanyika mapema leo jijini Dar.
Mchekeshaji Anne Kansiime anatarajiwa kutoa burudani kubwa siku ya Jumamosi kwa mashabiki
wake katika ukumbi wa Golden Tulip.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge, mkali huyo wa kuchekesha
na sanaa za majukwaani amesema mashabiki wake watarajie mambo makubwa hapo
Jumamosi.

‘Hii ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, hivyo mashabiki wangu watarajie burudani
ambayo itaacha mbavu zao hoi, lakini pia watapata nafasi ya kujifunza vitu
vingi kupitia vichekesho vyangu’ alisema Anne.

Kwa upande wake, mchekeshaji mwingine kutoka Kenya atayetoa burudani, Fred Omondi, amesema
watanzania watarajie burudani kali kama lilivyo jina la burudani yenyewe, Cheka
Kwa Nguvu. ‘Usiku wa Jumamosi utawakutanisha moja ya wachekeshaji mahiri barani Afrika, hivyo watanzania waje
kwa wingi kushuhudia burudani hii’ alisema Fred.

Naye mchekeshaji Pilipili kutoka Tanzania amesema usiku wa leo utakuwa usiku wa
kukumbukwa hasa kwa vichekesho alivyowaandalia mashabiki wake.Usiku
wa Cheka Kwa Nguvu unaandaliwa na kituo cha Radio 5 na pia utaambatana na burudani
ya muziki kutoka ODAMA Band. Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis amewataka
wapenzi wa burudani ya vichekesho kuhudhuria kwa wingi ili wafurahie burudani
waliyowaandalia.  ‘Usiku huo utakuwa ni maalumu kwa watanzania kufurahia Utanzania wao, kwani kucheka ni sehemu
muhimu kwa maisha ya mwanadamu’ alisema Robert.

Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka
vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto
mbalimbali za maisha.

Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye
kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini
Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...