
Mtuhumiwa
 wa Uwizi aliejitambulisha kwa jina la Juma Hamis huku akiwa na 
Kitambulisho cha Kazi cha Idara ya Usalama wa Taifa chenye jina la 
Kenedy Magige,akiwa amewekwa chini ya Ulinzi mara baada ya kunaswa Usiku
 huu kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam,

 Kitambulisho alichonashwa nacho Mtuhumiwa huyo kinaosomeka namna hii.


 Watuhumiwa hao wakiwa chini ya Ulinzi wa Polisi.

 Kitambulisho hicho kinavyoonekana kwa nyuma.

 Mtuhumiwa
 wa Uwizi aliejitambulisha kwa jina la Juma Hamis huku akiwa na 
Kitambulisho cha Kazi cha Idara ya Usalama wa Taifa chenye jina la 
Kenedy Magige.

 Mtuhumiwa
 mwenza wa Tukio hilo la Wizi,aliejitambulisha kwa jina la Takula 
Manyenga mwenye umri wa Miaka 28,akidhibitiwa kwa kufungwa kamba mara 
baada ya kukamatwa Usiku huu kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es 
Salaam.


 Watuhumiwa wote wawili wakipakiwa ndani ya Gari la Polisi kutoka katika Kituo cha Kawe,Jijini Dar es Salaam. 

 Watuhumiwa hao wakiwa ndani ya gari la Polisi.

 Askari Polisi wakiwa eneo la tukuo kuhakikisha Usalama unapatikana eneo hilo.

 Mara wakashushwa kwa muda na kuelekea kwenye Gari lao walilokuja nalo watuhumiwa hao.

 Askari
 Polisi wakiwa na Watuhumiwa hao wakati wakiendelea na Ukaguzi ndani ya 
Gari hilo aina ya Toyota Prado lenye nambari za Usajili T 445 BCY.

 Askari
 Polisi wakiendelea na Ukaguzi ndani ya Gari hilo,ambapo ndani ya Gari 
hilo kulikutwa na Simu zaidi ya kumi ambazo zilichukuliwa na Polisi hao.

 Gari walilokuwa wakilitumia Watuhumiwa hao.

 Wakipelekwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa safari ya kwenda Kituoni.

 Ulinzi mkali kwa watuhumiwa hao.

Msafara wa kuelekea kituoni.
Watu
 wawili wanaotuhumiwa kuwa ni wezi a.k.a Wapigaji/Matapeli wamekamatwa 
Usiku huu kwenye hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam.
Watu
 hao ambao wamekamatwa ni Bw. Takula Mayenga mkazi wa Mbezi Temboni na 
Bw. Juma Hamis ambaye ni mkazi wa Tabata wakiwa na nyaraka tofauti 
ikiwemo kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa, kadi za benki pamoja
 na simu zaidi ya kumi,wakiwa katika harakati za kumtapeli mwanadada 
mmoja aliejitambulisha kwa jina la Rebecca ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo 
cha Biashara cha CBE,Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaa  .
Akisimulia
 tukio dada huyo ambaye alipatwa na tukio hilo la kutapeliwa Ijumaa ya 
wiki iliyopita alisema kuwa, ilikuwa ni Ijumaa iliyopita wakiwa wamekaa 
katika fukwe wakipunga upepo ndipo alipokuja tapeli huyo na kukaa nao na
 baadae aliwawekea madawa ya kulevya na kuondoka na dada huyo kwenda 
kumtupa baharini.
