Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amefanya mabadiliko ya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera pamoja na baadhi ya Wakuu wa Upelelezi
wa mikoa na wakuu wa Polisi wa Wilaya katika baadhi ya mikoa hapa
Nchini.
Katika
mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa> Kagera,
Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Philipo Kalangi amehamishiwa Makao
Makuu ya Polisi Dar es Salaam, kuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia
usalama wa Mazingira na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Mayunga ambaye alikuwa Mkuu wa
kikosi cha kusimamia mazingira Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.
Aidha,
baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa (RCO) na wakuu wa Polisi wa
Wilaya(OCD) waliobadilishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa
makosa ya jinai mkoa wa Tabora ACP Edward Bukombe amehamishiwa Makao
Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Geita
(RCO) ACP Francis Kibona amehamishiwa mkoa wa Njombe kuwa mkuu wa
Upelelezi mkoa na nafasi yake inachukuliwa na SSP Simon Pasua kutoka
Makao makuu ya Upelelezi Dar es salaam.
Wengine
ni aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Wanging’ombe SSP.
Francis Maro amehamishiwa Mkoa wa Katavi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa
na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Katavi ACP. Emmanuel Nley
amehamishiwa kikosi cha Polisi wanamaji Dar es Salaam. Mkuu wa
Upelelezi mkoa wa Rukwa SSP. Peter Ngussa amehamishiwa Makao makuu ya
Upelelezi Dar es salaam, nafasi yake inachukuliwa na SSP Alan Bukumbi
aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa
Mkuu wa Polisi wilaya ya kati( OCD) Mrakibu wa Polisi (SP) Salum
Ndalama anaenda kuwa kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora na
aliyekuwa mkuu wa Polisi wa wilaya ya Tunduru (OCD) SP. Amadeus Tesha
anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Polisi reli. Uhamisho huo
ni wa kawaida katika kuboresha utendaji kwa mujibu wa kanuni, taratibu
na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.