Nay wa Mitego akiwpozi na warembo katika chumba cha hoteli moja maarufu jijini Nairobi nchini Kenya.
Mkali huyo ambaye anatamba na kibao ha Peleka Salam, amevujisha picha
hizo zinazomuonesha akiwa amezungukwa na warembo hao huku sehemu kubwa
ya mwili wake ukiwa wazi na nyingine kufunikwa na taulo.
Nay akiwa amezungukwa na warembo.
Aidha warembo hao nao walionekana kuchojoa viwalo vyao na kujifunika mataulo tu kuziba sehemu za miili yao.Nay wa Mitegho ambaye alienda Nairobi hivi karibuni na kukutana na wasanii kadhaa wa jijini humo ambao walimtembeza katika viwanja kadhaa vya starehe katika mishemishe za kujirusha na kugundua kwamba anakubalika sana nchini humo.
...Akichat kwenye simu katikati ya warembo hao.
Mwandishi wetu alimvutia waya, Nay wa Mitego ambaye amerejea nchini
hivi karibuni ili kutaka kujua sababu za kupiga picha hizo , msanii
huyo alikiri kuzipiga huku akikanusha kutenda ufuska wa aina yoyote ile.
...Mtu kati
“ Nilipokuwa Nairobi nimepiga picha nyingi kutokana na kuwa na
mashabiki wengi nchini humo lakini zipo nyingine ambazo kwa kweli si
nzuri ila nilizipiga kwa ajili ya video yangu mpya,” alisema Nay wa
Mitego.”