Home »
Uncategories »
TAZAMA HARUSI YA KIGOGO WA CHADEMA, HENRY KILEWO ALIYEFUNGA NDOA NA JOYCE KIRIA .... KIRIA AANIKA SIRI NZITO YA NDOA YAO HADHARANI .... SOMA ZAIDI
TAZAMA HARUSI YA KIGOGO WA CHADEMA, HENRY KILEWO ALIYEFUNGA NDOA NA JOYCE KIRIA .... KIRIA AANIKA SIRI NZITO YA NDOA YAO HADHARANI .... SOMA ZAIDI
Unknown
2:54 PM
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA
"MAELEZO YANGU HAYA YATAONDOA UTATA WOTE NA HOPE MTANIELEWA"
Kiruuuuuuuuuuuuuuuu wananchi wenye hasira kali angalieni msinitoe roho!
Kwa yeyote niliyemkwaza anisamehe bureeee..
Wacha niwape uzoefu-
1. Ndoa ya kwanza nilichangisha kama UTAMADUNI wa wengi kwenye jamii yetu...
Lakini Pamoja na michango tena mingi, tuliingia gharama zetu kubwa
sana, na kama haitoshi tulikopa. Baada ya shughuli tulianza KUPIGA MIAYO
YA NJAA hatuna ela na madeni juu..binafsi nilijuta sana lakini siku
zote MAJUTO ni Mjukuu...(siku isiyokuwa na jina Ndoaikasambaratikia****)
2. Ndoa ya pili.(BOMANI/SERIKALINI)Mungu akanikutanisha na Henry Kilewo
anaejua nini maana ya Mke, anaeniheshimu na kunitunza, anaenipenda na
kunijali.
Henry akaandaa sherehe NDOGO SANA ndugu
jamaa na marafiki WACHACHE sana, kwa GHARAMA ZAKE. Mume wangu Henry
Hakusumbua mtu yeyote. Baada ya lile tukio wala hatukupata ile adha ya
madeni na kuishiwa pesa kabisa ndani. Tukaendelea na maisha matamu kwa
Upendo na Uaminifu mpaka sasa.
3.KUMUHUSISHA MUNGU KWENYE TENDO/ KUBARIKI NDOA..
Kwa Mkristo hili ni tukio kubwa sanaaaaaa. Mungu wetu husamehe makosa
yoooote tunayotenda hapa duniani haijalishi! Ukirudi kundini
unasamehewa kila kitu. Ndivyo tulivyofanya jana tulirudishwa kundini
kisha TUKABARIKIWA. OOOH MY LORD JESUS THANK U SO MUCH KWA REHEMA NA
NEEMA. HAKUNA WA KUFANANA NA WEWE YEHOVA. kama Mungu amenisamehe wewe
ni nani hata unihukumu??. lets go back to the story
Ningekuwa na mawazo mgando ningefanya sherehe ya kukata na shoka..
kwanza kutetea jina langu(umaarufu mavi) na kuwazodoa waliochonga sana
kwamba kanisa nitalisikia kwenye tv na redio na magazeti)
Mazoea- kwa hiyo watu wengi huwa wanafanya sherehe kubwa sana
haijalishi anaanza au anaendelea ili KUWAFURAHISHA WATU WENGINE.....na
hasa akiwa na jina mjini Atajitutumua hata kama uwezo hana atafanya
kila awezalo aweke heshima uchwara mjini.
Mimi Joyce Kiria namshukuru Mungu amenipa Akili za Maisha siyo za
darasani za kukopi na kupesti. Nilizotumia wakati ule ikala kwangu!
Ningekuwa na Akili za kukopi na kupesti NINGEFANYA PATI KUBWA SANA BILA
KUCHANGISHA MTU kwa sasa namshukuru Mungu si haba uwezo wa sherehe
ninao, NA HATA NINGEAMUA KUCHANGISHA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI NINGEPATA
PESA NYINGI SANA KWA TAARIFA YAKO.
HITIMISHO.
TZ ndo nchi iliyobaki tunachangisha sherehe. Jirani zetu wanachangia ugonjwa na Elimu. Tukubali kubadili mitazamo yetu.
Kama unauwezo wa kufanya Sherehe fanya kwa sababu ni jambo jema sana. Usiwasumbue watu kwa michango. Haina maana hata kidogo.
Kwa sisi ambao hata uhakika wa maisha bora hatuna, tunaishi tu bora
kumekucha tunamshukuru Mungu, siyo lazima tuchangishe watu, tujikite ktk
kuboresha maisha yetu ili baadae tufanye sherehe bila kutegemea
michango, michango ni shida kubwa sana. Kama kuna watu waliomaliza
salama bila kubaki na umasikini ni wachache sana...
Au
tuendelee kuchanga lakini hizo fedha zikatusaidie kwenye maisha.
Wahusika wakaanzishie miradi ya kuwasaidia. Siyo kula kunywa na kucheza
kwaito hapana aiseeeee...
Pia jana tulibatiza Watoto wetu ambao Tunawapenda sana. Tungeweza pia kufanya sherehe kubwa...
Kwa kuwa hatukufanya Sherehe na uwezo tunao, mwakani tutawapeleka Shule
watoto kadhaa wenye uhitaji kwenye jamii yetu. Yule binti aliyeshindwa
kufanya mtihani wa 4m4 kule rombo, tutampeleka private kwa sababu
walisema hawana uwezo huo ndo maana alikuwa tayari kuendelea kusoma
wakati mtoto akiwa na wiki kadhaa toka azaliwe, wale watoto 3 wa Stela
aliyekatwa mkono huko dodoma kama unawakumbuka, watoto 2 wa Gati Chacha
aliyekatwa mguu huko Tarime Mara n.k
Tuchangie maendeleo tuachane na sherehe....Kenya wameweza kwa nini TZ tushindwe?!
Wanangu nitawasihi sana wasifanye SHEREHE bali wasaidie wengine au
waanzishe miradi na kama wana uwezo basi wafanye bila kuathiri uchumi
wao na wasisumbue watu.
Joyce kiria
Mwanamabadiliko
Nawapenda wote....