ZIARA YA KATIBU MKUU DK WILLIBROD SLAA

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa ataanza ziara ya siku 20 katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida kuanzia Desemba 4-23, mwaka huu.
Lengo la ziara hiyo ambayo imetokana na maombi ya muda mrefu ya viongozi wa chama katika maeneo husika, ni kuimarisha na kukagua uhai wa chama katika ngazi za chini hususan kata na majimbo mikoa hiyo.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakutana na wananchi katika mikutano ya hadhara ambapo atazungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa na eneo husika, kisha atafanya vikao vya ndani vya kichama.
Ziara hiyo itaanzia mkoani Shinyanga ambapo siku ya Jumatano Desemba 4, mwaka huu, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Wilaya ya Kahama, siku inayofuata Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe.
Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwa vyombo vya habari.
Imetolewa Jumanne, Desemba 3, 2013, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...