AJALI YAUA WAWILI, YAJERUHI 23 MKOANI MBEYA

Hivi ndivyo ilivyokuwa ajali hiyo iliyohusisha Lori na Coaster katika eneo la Mbalizi.

Baadhi ya wananchi wakishuhudia ajali hiyo iliyotokea leo jioni katika eneo la Mlima Iwambi kuelekea Mbalizi.

Baadhi ya askari polisi wakilinda mali zilizokuwemo katika lori, hata hivyo askari hao walilazimika kurusha risasi hewani kuwatawanya watu waliotaka kupora bidhaa hizo.

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya akisubiri kupatiwa matibabu.
WIMBI la ajali katika miezi ya Disemba na Januari nchini limeendelea baada ya ajali nyingine kutokea mkoani Mbeya leo jioni majira ya katika mteremko wa Mbalizi na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine 23.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ni kwamba magari mawili moja aina ya Coaster na Lori la mizigo yalikuwa yakielekea njia ya Tunduma kutokea Jijini Mbeya ambapo lori hilo linadaiwa kuharibika mfumo wa breki likiwa mteremkoni.
Lori hilo la mizigo aina ya Scania lenye namba za usajili T 101 CRL na tela lenye namba za usajili T 859 BZW ambalo lilibeba bidhaa mbalimbali za madukani liliigonga Coaster yenye namba za usajili T 910 BFB na kusababisha magari hayo kupinduka.

(Picha kwa hisani ya Charles Abraham wa Malafyale Blog)


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...