Zitto Kabwe aweka pingamizi Mahakamani kuzuia Kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kumjadili


Mbunge wa Kigoma Kaskazini  kwa tiketi ya  Chadema, Zitto Kabwe leo ametinga Mahakama Kuu ya Tanzania,Kanda ya Dar es Salaam kuweka pingamizi la kisheria kuzuia Mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA uliopangwa kufanyika kesho tarehe 3/1/2014.

Zitto kupitia kwa Wakili wake Albert Gabriel Msando,aliwasilisha pingamizi hilo kwa Hati ya dharura iliyosainiwa na Wakili Msando. Pingamizi hilo limesikilizwa leo na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Jaji Uttamwa.CHADEMA iliwakilishwa na jopo la Mawakili lililoongozwa na Wakili Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA.

Hoja za Zitto zililenga kuzuia mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA uliopangwa kufanyika kesho ukiwa na ajenda tatu ikiwamo kupokea utetezi wa mdomo wa wanachama watatu wa CHADEMA wanaotuhumiwa kukiuka Kanuni na Taratibu za chama: Zitto,Samson Mwigamba na Dr.Kitila Mkumbo.

Hoja za Zitto ni kuwa kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA cha kesho kitazuia kusikilizwa kwa rufani yake aliyoiwasilisha Baraza Kuu akipinga kuvuliwa kwake nyadhifa ndani ya chama bila ya kusikilizwa. Hii ni kusema, Zitto alishaadhibiwa bila ya kujibu tuhuma dhidi yake.

Wakili  Msando,kiujumla, amejenga hoja kuwa kikao cha CC ya CHADEMA cha kesho kisijadili jambo lililokwisha kukatiwa rufaa na hivyo rufaa isikilizwe kwanza na Baraza Kuu. Ya kwamba, tuhuma 11 ni tuhuma mpya na tayari Zitto ameshaadhibiwa pasipo kutenda jambo lolote na kusikilizwa popote.

Source: Jamii Forum


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...