 Staa wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans.
Staa wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans.STAA wa sinema za Kibongo, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufundishwa mila za kimasai na kusema ameelewa, muda mchache baadaye akachemka.

Chuchu Hans (kushoto)katika pozi.
Tukio hilo lililogeuka kituko, lilitokea hivi karibuni ambapo Chuchu 
akiwa na wasanii wenzake walifika katika Kijiji cha Misherani kilichopo 
mkoani Arusha kwenda kurekodi sinema lakini alivutiwa na mavazi ya 
kimasai ndipo alipoomba kujifunza mila za kabila hilo. Akizungumza
 paparazi wetu, Chuchu alisema alipewa mtoto mdogo amfundishe namna ya 
kuvaa mavazi hayo ya Kimasai, akadai ameweza lakini alipopewa mara ya 
pili avae mwenyewe, alichemka.
Akizungumza
 paparazi wetu, Chuchu alisema alipewa mtoto mdogo amfundishe namna ya 
kuvaa mavazi hayo ya Kimasai, akadai ameweza lakini alipopewa mara ya 
pili avae mwenyewe, alichemka.“Daah! Niliabika maana mbaya zaidi nilielekezwa na binti mdogo nikamwambia tayari nimeweza lakini nilipokwenda kuvaa, nikavaa ndivyo sivyo, acha nichekwe,” alisema Chuchu.

Chuchu Hans (wa poli kutoka kulia) na watoto wa Kimasai.
Hata hivyo, baada ya kukosea huko, Chuchu alisema alijifunza upya na 
kuhakikisha kuwa ameweza hivyo kufuta aibu ya awali huku akiwasisitiza 
wasanii wenzake kujifunza mila tofautitofauti. “Kujivunza
 mila tofauti ni jambo zuri katika maisha yetu hususan sisi wasanii, 
tunatakiwa kujua milia na tamaduni za kabila mbalimbali ili 
kuyawakilisha katika sinema zetu,” alisema Chuchu
“Kujivunza
 mila tofauti ni jambo zuri katika maisha yetu hususan sisi wasanii, 
tunatakiwa kujua milia na tamaduni za kabila mbalimbali ili 
kuyawakilisha katika sinema zetu,” alisema Chuchu