Mike Lukindo enzi ya uhai wake.
Watanzania
wa Wisconsin wanapenda kutoa shukurani kwa wote waliojaribu kuokoa
kutokuchomwa moto kwa ndugu yetu, mpendwa wetu Mike Lukindo na pamoja na
jitihada zote zilizofanyika tunasikitika kuwataarifu kwamba mpendwa
wetu ilibidi achomwe moto na jana Ijumaa April 4, 2014 majivu yake
walikabidhiwa familia yake kwa mtoto wa kwanza wa marehemu kwenda
kuchukua majivu hayo. Mpaka mazishi yafanyike zilikua zinahitajika
$6,000 pamoja na michango ya sisi tuliopo Madison, Wisconsin haikuweza
kufikia idadi iliyokua inahitajika.
Watanzania
wa Wisconsin wanawashukuru vyombo vya habari ndani na nje ya Marekani
vilivyosaidia kusambaza habari ya ndugu yetu, mpendwa mwenzetu na
Mtanzania mwenzte mpaka habari kuwafikia ndugu zake Tanzania.
Shukurani
za pekee kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani hususani Mhe. Balozi
Liberata Mulamula kwa mchango waliotoa na mara kwa mara Balozi kupiga
simu kufuatilia maendelea ya msiba.
Sisi Watanzania wa Wisconsin kwa niaba ya familia tunasema asante na mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atawazidishia, Asanteni.