Mchezaji wa 
timu ya taifa ya Ivory Coast ambaye pia anaichezea klabu ya Manchester 
City, Yaya Toure amesema kuwa asili yake ya uafrika ni kigezo kikubwa 
kinacho mfanya ashindwe kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Toure 
alisema kuwa mashabiki wengi wa ulaya hususan ni uingereza hawamthamini 
sana kwa kuwa ni muafrika.

Akiongea na 
City Tv, Toure alisema ''ukija Afrika ukiuliza jina Messi kila mtu 
atakwambia anamjua lakini ukienda ulaya na kuuliza jina Yaya Toure watu 
watakuuliza, Yaya Toure ni nani? Hali hii inaonesha kuwepo kwa ubaguzi 
wa hali ya juu katika soka la ualaya, alisema Yaya. 
Baada ya kunyakua kombe cha Capital One katika dimba la Wembley mnamo mwezi Machi, mchezaji Samir Nasri ambaye pia ni kiungo wa Manchester City alisema ''Yaya Toure ni mchezaji ambaye anastahili kuwa kiungo bora wa dunia kama asingekuwa muafrika'' kauli hiyo ya Nasri iliungwa mkono na kiungo huyo raia wa Ivory Coast '' nafikiri alichokisema Nasri ni kweli kabisa'' Yaya Toure aliwaambia waandishi wa habari wa bbc.
Yaya Toure ni mmoja kati ya wachezaji sita waliochaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka katika soka la Uingereza maarufu kama '' Professional Footballers' Association (PFA)'' ambapo atashindana na miamba mingine kama Steven Gerrard, Daniel Sturridge and Luis Suarez, Eden Hazard and Adam Lallana na mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa Aprili 27.
Toure 
amewahi kushinda vikombe vya ligi akiwa Uispaniola, Uingereza na Ugiriki
 pia aliwahi kunyakua kombe la mabingwa ulaya akiwa na Barcelona.
