
Kutokana 
na mjadala wa bajeti ya wizara ya mambo ya nje uliokuwa unaendelea , 
Mbunge wa Nkasi Ndugu Ali Kessy ameporomosha matusi mazito kwa 
wazanzibar kuwa ni watu wa hovyo na ambao kila mara wanalialia tu kuwa 
wanabaguliwa , wanadai mambo mengi kuliko uwezo wao na wakati 
hawachangii hata senti kwenye Muungano na hivyo kama wanaona wanaonewa 
waende kwenye nchi yao sio kukaa kwetu..
Alienda 
mbali zaidi kusema kuwa Zanzibar Majimbo ya uchaguzi ni madogo kiasi 
kwamba ukipigania filimbi wananchi wote wanakusanyika ila bado wanapewa 
fedha za mfuko wa Jimbo jambo ambalo sio haki , na pia hata umeme 
hawalipi na maji pia .
jambo 
hili lilimfanya mbunge wa CCM ndugu Chombo , kuomba muongozo na Kumtaka 
naibu Spika a mwambie Kessy kamwe asikanyage Zanzibar , hii ilikuwa 
baada ya kumuita mwendawazimu , na alisema ni bahati mbaya kwa CCM kuwa 
na mbunge mwendawazimu kama huyu ......
Ndugai muda muda wote alikuwa akicheka , sijui nini maana yake .."...
