Mtuhumiwa Mtonga Omari akitoka mahakamani huku 
mikono
 ikiwa kichwani akijutia Unyama anayodaiwa  kumfanya mtoto huyo wa 
marehemu shemeji yake aliyefahamika kwa jina la Mwasiti Said.
Watuhumiwa wa 
mtoto anayedaiwa kufichwa kwenye boksi, wamefikishwa katika Mahakama ya 
Hakimu Mkazi  mjini Morogoro, kujibu mashtaka ya kula njama na kufanya 
ukatili dhidi ya mtoto huyo.watuhumiwa
 hao waliofikisha mahakamani hapo chini ya Ulinzi mkali ni Rashid Mvungi
 (47), washtakiwa wengine katika kesi hiyo iliyovutia umati wa watu wa 
mji wa Morogoro ni mama mlezi wa Nasrah, Mariamu Said (38) na mume wake 
Mtonga Omar (30).
Baba
 mzazi wa Nasra Bw Mvungi aliyevaa shati la karoakiingia kwenye mahabusu
 ya mahakama ya mkoa akisubiri kupelekwa gerezani baada ya kushinda 
kutimiza masharti ya dhamana,Wananchi waliokuwepo mahakamani hapo 
walifurahia watuhumiwa hao kupelekwa magereza baada ya kushindwa 
kutimiza masharti ya dhamana.
Hatimaye wale 
Washtakiwa
 hao walifikishwa katika mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi 
Mfawidhi Mary Moyo, Jumatatu ya wiki hii  na kusomewa mashtaka hayo.
Wakili
 wa Serikali, Sunday Hyera alidai kuwa washtakiwa  walitenda makosa hayo
 kati ya Desemba mwaka 2010 na Mei mwaka huu katika mtaa wa Azimio kata 
ya Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro.
 Wakili
 huyo alidai kuwa katika kipindi hicho, washtakiwa wakiwa walezi wa 
mtoto Nasrah, walimfanyia ukatili wa mtelekeza na kumpa malezi akiwa 
ndani ya boksi na hivyo kumsababishia magonjwa.
Wakili
 huyo wa Serikali, aliyataja maradhi yaliyokumba mtoto huyo akiwa ndani 
ya boksi kuwa ni pamoja na utapiamlo, maumivu ya kifua na mvunjiko wa 
mifupa katika mwili wake.
Hyera alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama kutaja tarehe ya kuisikiliza.
Hata hivyo Wakili huyo aliiomba mahakama kuwa upande wa Jamhuri hauna kipingamizi kuhusu dhamana kwa washtakiwa.
Mahakama
 chini ya hakimu wake Moyo, ilisema dhamana kwa washtakiwa iko wazi 
lakini kwa masharti ya kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili 
watakaosaini bondi ya Sh5 milioni kila mmoja.
Alisema  sharti lingine ni wadhamini kuwa na barua kutoka kwa waajiri wa kuaminika au serikali za mitaa.
Hata hivyo washtakiwa walishindwa kutimiza masharti hayo, hatua iliyowafanya warejeshwa gerezani
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 9 mwaka huu itakapotajwa tena..
