
Dakika
 kadhaa baada ya mshindi wa tuzo ya BET 2014 kwa wasanii wa Afrika 
kutangazwa kuwa Davido wa Nigeria, staa kutoka Tanzania Diamond Platnumz
 aliekua anawania pia tuzo hiyo ameandika ya moyoni kwa watu 
wake.Tusipopenda kukubali matokeo na ushindi wa wenzetu basi daima 
hatutaweza kuwa
washindani,
 muhimu ni kujua wapi tulipotoka na wapi tulipo leo, katika nchi zaidi 
ya 20 zenye wasanii zaidi ya milioni 40 kuchaguliwa Tanzania ni fursa, 
heshima na hatua kubwa, cha muhimu ni kuitumia vyema fursa hii na 
kuhakikisha mwakani tunapiga hatua, asante sana kwa wote wanaozidi 
kunisupport’

