JAMBO limezua jambo! Yule jamaa aliyefahamika kwa jina la Huruma Bernard ambaye alidai kumfumania baba mwenye nyumba wake, Lugali akitaka kuvunja amri ya sita na mkewe, hatimaye ameamua kuhama nyumba.Fumanizi hilo liliripotiwa wiki iliyopita ambapo Huruma alimfumania baba mwenye nyumba huyo kwenye gesti moja iliyopo Buguruni, Dar.
Bw. Huruma Bernard ambaye alidai kumfumania baba mwenye nyumba wake, Lugali akihama na mkewe kutoka nyumba waliyopanga.
Katika
tukio la kuhama, Ijumaa iliyopita, wanahabari wetu walitonywa na chanzo
chao kuwa Huruma alikuwa anahama katika nyumba aliyokuwa anaishi maeneo
ya Ukonga, Dar baada ya kupewa notisi na baba mwenye nyumba huyo ili
kuondoa fedheha ya kumfumania gesti na mkewe.
...Mke na mume walifunga virago vyote tayari kwa kuhama.
Wanahabari
wetu walipofika eneo hilo walimkuta Huruma na mkewe wakibeba vitu
ambapo jamaa huyo alisema kuwa amekubali kuondoka kwenye nyumba hiyo
baada ya kuona hakutakuwa na maelewano tena.
...Mke na mume wakiwa nje ya nyumba waliyopanga.
“Nimekubali kuhama kwani maelewano na baba mwenye nyumba hayakuwa mazuri tena baada ya kumfumania na mke wangu,” alisema Huruma.
...Mke na mume hao wakiondoka.
Alisema
kwamba mkataba wake katika nyumba hiyo ulikuwa unatakiwa umalizike Machi
Mosi, mwakani lakini baada ya kumfumania wamekuwa na bifu kubwa kiasi
cha kukaribia kutwangana kila wanapopishana.
Shauri lao bado lipo kwenye Kituo cha Polisi cha Buguruni likiwa na
faili la kesi namba BUG/RB/6182/ 2014- UTEKAJI kwani baada ya fumanizi
jamaa huyo alidai alitekwa