Wananchi wa Mlangali Ludewa wakiwa wamekizingira kituo cha polisi Mlangali mara baada ya kuipeleka maiti ya mtoto aliyeteketea kwa moto katika kituo hicho |
Wananchi Mlangali Ludewa wakiwa wamekizingira kituoa cha polisi cha Mlangali jana |
Kitanda ambacho mtoto huyo alikuwa amelala |
Dirisha likiwa limevunjwa ili kuutoa mwili wamtoto aliyeungua kwa moto |
Wananchi wakitazama chumba alichokuwa amelala mtoto huyo aliyeteketea kwa moto |
Nyumba ya askari iliyodaiwa kutumika kufanya mapenzi na mwanafunzi huyo kabla ya mtoto kutetekea kwa moto
.................................................................................................................
KIONGOZI
wa mbio za mwenge Kitaifa awatuliza wananchi wa Mlangali wilaya ya
Ludewa ambao baadhi yao waliandamana kituo cha polisi kushinikiza
kutolewa kwa askari polisi aliyedaiwa kusababisha kifo cha mtoto ili
auwawe .
kiongozi huyo aliwaomba wananchi wa Mlangali kutokubali kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na kuepuka kujichukulia sheria mkononi kutokana na wananchi zaidi ya 200 jana kuvamia kituo cha polisi Mlangali na kuacha kushiriki mbio za mwenge kutokana na mmoja kati ya askari kudaiwa kusababisha mauwaji ya mtoto wa miaka 2.
Mbali ya kiongozi huyo kuwaomba wananchi kutofanya vurugu hizo na kutaka kuacha vyombo vya usalama kulifanyia kazi bado wananchi hao waliendelea kukizunguka kituo hicho cha polisi hadi majira ya mchana huku mwili wa mtoto huyo ukiwa umepelekwa kituoni hapo baada ya kuungua vibaya kwa moto.
Wananchi hao walifikia hatua hiyo ya kuzingira kituo cha polisi kutokana na kifo cha mtoto Angela Mtitu kufariki dunia kwa moto wakati askari polisi aliyetambuliika kwa jina moja la kabasa kudaiwa kumrubuni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule moja ya sekondari wilayani Ludewa ambae ndie alikuwa akimlea mtoto huyo na kwenda kufanya nae mapenzi nyumba ya pili ambako ni nyumbani kwa askari huyo na kupelekea mtoto huyo kuungua moto.
Hivyo wananchi hao wenye hasira kali walilazimika kukizingira kituo hicho kwa zaidi ya masaa matano kabla ya askari wa FFU kutoka mkoani Njombe kufika eneo hilo na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi huku mwili wa mtoto huyo ukiwa ndani ya kituo cha polisi pamoja na askari huyo na binti huyo mwanafunzi ambao walikuwa wakishikiliwa na jeshi la polisi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe hakuweza kupatikana kuzungumzia undani wa tukio hilo japo baadhi ya askari waliokuwepo eneo la tukio walidai kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia.
Mtandao
huu www.jamvilahabari.com ulifanya mawasiliano na baadhi ya wananchi
hao walidai kuwa baba wa mtoto huyo alikamatwa na polisi kwa kesi ambayo
ambayo haipo wazi lakini wanadai mzazi huyo kuwekwa kizuizini ni mbinu
ya askari huyu ili aendelee kujivinjari na mwanafunzi huyu wa Ulayasi
sekondari.
Pia
katika vurugu hizo inadaiwa askari wa kutuliza ghasia walitumia mwanya
wa vurugu hizo kupora mali katika baadhi ya sehemu za biashara.
Wananchi hao wamesema walikwenda polisi
kuripoti kupotelewa kwa mali zao wanadai mkuu wa kituo anasema hawezi
kupokea malalamiko yao kwakuwa jambo hili lipo ngazi za juu, kituhicho
kimewafanya wanachi hao washindwa kuelewa wapi ni sehemu sahihi
yakupeleka malalamiko yao.