Wapelelezi
wa Uingereza wanafanya uchunguzi juu ya tukio la kukaribia kugongana
kwa ndege mbili aina ya Jumbo Jet hivi karibuni kwenye anga ya Scotland
ambapo ndege hizo aina ya Jumbo Jet 747 zilikaribia kugongana zikiwa
hewani saa chache baada ya kupaa huku zikiwa zimebeba abiria zaidi ya
elfu moja
Waongozaji
wa ndege hizo wanasema kuwa marubani wa ndege hizo hawakufuata
maelekezo sahihi ambapo rubani mmoja aliomba kupewa maelekezo na
alielekezwa kwenda kuifuata ndege nyingine jambo ambalo lingesababisha
ajali mbaya, marubani wote waliona ndege mbele yao.
Unaambiwa
aliekuepo chumba cha kuongozea ndege alikubali ombi la mmoja wa marubani
kwenye ndege lililotaka ruhusa ya kutumia njia ya juu kwenye anga na
akaruhusiwa lakini kumbe aliekua kwenye hicho chumba hakujua kwamba kuna
ndege nyingine ambayo ilikua inatumia hiyo njia.
Baadae ndio
muongozaji kwenye hiki chumba cha kuongozea ndege alishtuka ndio mipango
ya kuziondoa hizi ndege kwenye njia moja ikaanza…. ilikua hekaheka
ambapo walifanikiwa kuziokoa ndege kutogongana na zikakwepana kwa umbali
mdogo sana.
Mara ya mwisho kwa ndege za Marekani kuponea chupuchupu kugongana zikiwa angani kama hivi ilikua ni mwaka 1978.