WASANII wa filamu, Ruth Suka ‘Mainda’ na Salome Ndumbagwe Mesayo ‘Thea’ sasa wameonekana kujikita zaidi kwenye mafunzo ya kiroho baada ya hivi karibuni kunaswa kwenye kongamano la ukombozi ndani ya Ukumbi wa Vatican City Sinza jijini Dar walipokwenda kuabudu.
Salome Ndumbagwe Mesayo ‘Thea’.
“Sisi tumempokea Yesu, tunawasihi wasanii wenzetu waachane na
ushirikina waje huku ambako kuna njia salama, hili ni kongamano ambalo
lina mafunzo mema na lina uwezo wa kumbadili mtu kutoka kwenye roho ya
kishetani na kuwa na roho safi,” alisema Thea.